Tuesday, 5 January 2016

MANUFAA YA TANGAWIZI KWA KUTULIZA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI

Mara nyingi wnawake wengi wakati wa hedhi, huhisi maumivu kidogo na kusababisha kukosa raha na kushindwa kabisa hata kufanya shughuli nyingine muhimu.

Baadhi ya wanawake wanapokaribia kuingia katika siku zao misuli hubana na maumivu ya mapaja na miguu.

Lakini wakati mwingine hali huwa inakuwa mbaya zaidi ambapo mhusika anapata maumivu makali ya mgongo, tumbo na hata maumivu wakati wa kutoa damu.

Sasa basi Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kwamba tangawizi inaweza kuwa suluhisho la tatizo la maumivu hayo makali wakati wa hedhi kwako mwanamke.

Unachotakiwa kufanya ni kupondaponda tangawizi mbichi, kisha chemsha maji ya kutosha kwa dakika kumi. Ongeza sukari kidogo halafu chuja.

Tumia glasi moja ya maji hayo mara tatu kwa siku hususani mara baada ya kula.

Matibabu haya ni vyema yakaanza siku tatu kabla ya hedhi na kipindi chote cha hedhi.

Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi, lakini kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic, Tabibu, Abdallah Mandai kila siku ya Jumatatu hadi Jumapili ofisi kwake , Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment