Saturday, 2 January 2016

MAWAZIRI WATATU WATEMBELEA MACHINJIO YA VINGUNGUTI NA KUWASIMAMISHA KAZI BAADHI YA WATUMISHI WA UMMAMawaziri watatu wakiongozwa na waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi utumishi na utawala bora wamefanya ziara katika machinjio ya Vingunguti na kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa umma kwa madai ya kuwepo kwa ufisadi wa mali za umma.

George Simbachawene amewaongoza mawaziri wengine ambao ni waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Afya Hamisi Kigwangala kufanya ziara katika machinjio hayo na kubaini matatizo mbalimbali ikiwamo ukiukwaji wa taratibu za kulipia ushuru kwa wanyama ambapo ilibainika idadi ya mbuzi ama ng'ombe wanaolipiwa ili kuingia katika machinjio hayo nitofauti na vibali vinavyotolewa ambapo waziri wa mifugo alitoa mfano wa jana alipofanya ziara ya kushtukiza usiku alikuta kuna vibali vya mbuzi miatatu lakini idadi ya mbuzi waliyokuwepo ni zaidi ya miasita.

Naye waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi George Simbachawene alitaka kufanyika uchunguzi wa kina ili kubaini gharama za kutengeneza vibanda vya kuwekea nyama ambavyo vilidaiwa kutengenezwa kwa gharama ya shilingi milioni miamoja jamboa ambalo hakukubaliana nalo,huku naibu waziri wa afya akimtaka waziri huyo wa Tamisemi kuondoka na daktari wa eneo hilo kwa madai kushindwa kazi na kugubikwa na masuala ya ufujaji wa mali za umma.

No comments:

Post a Comment