Monday, 4 January 2016

NAMNA VYAKULA VINAVYOWEZA KUJENGA AU KUBOMOA AFYA ZETUHabari za Jumatatu ya Januari 04, 2016 mdau wangu wa www.dkmandai.com sina shaka utakuwa upo vizuri karibu tuendelee kuyafahamu haya mengine zaidi kuhusu afya zetu.

Siku zote mitindo ya maisha tunayoishi na namna tunavyokula huweza kutusababishia kuzibomoa afya zetu na kujikuta tunapata magonjwa mbalimbali hasa yale yasiyoambukizwa.

Siku za hivi karibuni magonjwa kama matatizo ya moyo, kisukari, saratani yamekuwa yakiwakabili watu wengi zaidi na hii ni kutokana na sababu ya ulaji hovyo wa vyakula suala ambalo kwa ujumla wake linaingia katika mtindo wa maisha.

Leo kupitia Mandai Herbalist Clinic tumeona ni vizuri tukuletee orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo vinaaminika kusababisha magonjwa hatari

Matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi

Vyakula vyenye chumvi nyingi huweza kusababisha saratani, kwani inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa saratani tumboni. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni kama vile vya kusindika, mfano nyama za makopo, maharage pamoja na kiwango cha chumvi kinachoungwa jikoni wakati wa kupika.

Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula vya kukaanga
Mara nyingi vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya, ikiwa ni pamoja na mhusika kuwa na uwezekano wa kuweza kupata saratani ya kwenye mfuko wa uzazi. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na 'chips' 'sausage' na vingine ambavyo hupikwa kwa namna hiyo.

Matumizi ya sukari kupita kiasi.
Matumizi mabaya ya sukari yamekuwa yakielezwa kusababisha saratani. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa katika vinywaji mbalimbali, mfano juisi soda, mara nyingi vinywaji hivyo huwa na sukari nyingi inayoweza kupelekea saratani ya kongosho. Sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula

Matumizi ya pombe
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao huweza kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake na waume. Aina ya saratani zinazowezwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya ini, utumbo na koromeo.

Matumizi ya nyama na mafuta
Watu wanaopenda kula nyama kila siku, huweza kuwa katika hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja.

Hivyo ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kukusababishia maradhi mbalimbali na hasa ya saratani, hivyo ni vizuri kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku.

Kama unahitaji ushauri au unamaoni zaidi unaweza kupiga simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment