Saturday, 9 January 2016

PICHA RASMI YA RAIS DKT MAGUFULI TAYARI IMETOKA IPO HAPA


Picha rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli imeshatoka katika ofisi ya idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo  Bi Zamaradi Kawawa kuwa picha hiyo itauzwa kwa shilingi 15,000 ya kitanzania bila ya kuwekwa fremu, huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa kwa shilingi 5000/=

Bi Kawawa amesema nakala za picha hiyo zinapatikana Idara ya Habari Maelezo na ofisi za wakala wa huduma ya ununuzi serikalini (GPSA)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo  Bi Zamaradi Kawawa (kushoto) akiwa na Mkurugenzi msaidizi wa habari maelezo Raphael Hokororo wakionesha kwa waandishi wa habari picha rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

Mbali na hayi Bi Kawawa amesema picha hiyo ya Rais pamoja na ya baba wa taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Maashirika na Taasisi binafsi.

Naye Mkurugenza msaidizi wa habari maelezo Raphael Hokororo amesema picha hiyo ya Rais Magufuli imwahi kutoka kuliko picha za waheshimiwa wote waliopita na kusema kuwa hairuhusiwi kukopi au kunakili picha hiyo.
i
Hokororo  pia ametoa onyo kwa wote wanaosambaza picha isiyo rasmi na wale wote wanaotengeneza picha yenye ukubwa usio rasmi nakusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Idara ya Habari Maelezo pekee ndiyo yenye hakimiliki ya picha picha hiyo," alifafanua Bw. Hokororo


No comments:

Post a Comment