Thursday, 7 January 2016

SIFA ZA MAJANI YA MPERA KATIKA MATIBABU

Unapokula chakula mara zote huwa unatarajia kufurahia chakula na si kupata karaha, lakini kuna wakati chakula huweza kuwa kikwazo hasa pale unapokula na kupata kichefuchefu na hatimaye kutapika.

Kutapika hutokana na tatizo ndani ya mfumo wa uyeyushaji wa chakula (digestive system). Kichefuchefu na kutapika mara nyingi huwa na uhusiano na mfumo wa uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo.

Iwapo kutapika kutakuwa kumesababishwa na mzio wa chakula, kula kuzidi kiasi au sumu ndani ya chakula, ni vyema kutapika kuendelee badala ya kuzuia ili chakula chote kilicho tumboni kitoke kwani baada ya kutapika hali itarudi kuwa ya kawaida.

Sasa pale endapo utaona kuna umuhimu au haja ya kuzuia kutapika ili kukinga athari kubwa zinazoweza kujitokeza baadaye:

Unaweza kutumia majani ya mpera ili kuzuia tatizo la kutapika unachopaswa kufanya ni kuchemsha majani ya mpera kwa muda wa dakika ishirini.Kisha kunywa nusu glasi ya maji hayo ili kuzuia kutapika. Rudia tiba hiyo baada ya saa moja hadi kutapika kutakapokoma.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaiz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment