Monday, 11 January 2016

TUMIA MANJANO (BINZARI) KUTIBU MATATIZO YA MAUMIVU YA MIGUU


Maumivu ya miguu ni moja ya tatizo ambalo limekuwa likiwakabili watu wengi kwa sasa, miaka ya nyuma tatizo hili lilikuwa likiwakabili zaidi watu wenye umri mkubwa, lakini kwa sasa tatizo hili limekuwa likiwakabili hata vijana pia.

Tatizo hili huweza kuwa ni la mguu mmoja au hata miguu yote miwili na sababu za matatizo haya huchangiwa na uchovu wa misuli, ukosefu wa lishe bora, upungufu wa maji mwilini au kusimama kwa muda mrefu.

Sasa basi kutokana na tatizo hili kuwasumbua wengi hapa napenda kukwambia kwamba manjano huweza kutatua tatizo hili endapo yakitumika vizuri.

Kinachohitajika kufanyika ni kijiko kimoja cha unga wa manjano pamoja na mafuta ya ufuta kisha changanya kidogo halafu tumia mchanganyiko huo kupaka sehemu yenye maumivu.

Baada ya kupaka mchanganyiko huo kaa nusu saa kisha nawa vizuri kwa maji ya uvuguvugu na ufanye zoezi la kutumia mchanganyiko mara mbili kwa siku.

Kabla ya kutumia njia hii ya kimatibabu ni vyema kupata ushauri wa Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment