Friday, 1 January 2016

WADAU WA TIBA ASILI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu jana alikutana na wadau wa tiba asili ofisini kwake na kufanikiwa kujadili mambo mbalimbali.

Pamoja na kukutana huko imeelezwa kuwa wiki ijayo watatoa tamko kuhusiana na majadiliano hayo ambayo yalionekana kwenda vyema.

Haya yote yanafuatiwa na taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Wizara ya Afya yenye agizo linalowataka waganga wote wa tiba asili wenye vibali vya kutoa huduma hiyo kuwasilisha vibali hivyo katika Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa ajili ya kuvipitia upya vibali hivyo.

Katika agizo hilo la serikali imetoa siku 14 kwa watoa huduma wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini kuwa wamewasilisha nyaraka zao zote zinazowaruhusu kutoa huduma hiyo na ziwasilishwe kwenye baraza hilo.

Hapa chini ninazo picha za pamoja za wadau wa tiba asili wakiwa pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


No comments:

Post a Comment