Saturday, 2 January 2016

YATUMIE MAJANI YA UKWAJU KUTIBU KIKOHOZINapenda kuendelea kusema Happy New Year mdau wangu wa www.dkmandai.com naomba pia tuendelee kujuzana mambo haya muhimu kuhusu tiba asili.

Sasa leo naomba tuangazie majani ya ukwaju ambayo huweza kumsaidia mtu ambaye anasumbuliwa na kikohozi kwa muda mrefu.

Kuna baadhi ya watu hujikuta wakisumbuliwa sana na kikohozi tena kwa muda mrefu na wakipima hujikuta hawana kabisa tatizo la kifua kuu. Sasa basi kama wewe ni miongoni mwa watu wa namna hiyo hebu jaribu tiba hii pia.

Tafuta majani ya ukwaju kiasi cha fungu moja la mboga za majani, kisha yatwange halafu weka maji robo lita katika majani hayo yaliyotwangwa na kisha koroga vizuri.

Ukishapata mchanganyiko huo, utahitajika kutafuta asali kwenye ujazo wa kikombe kidogo cha chai kisha changanya na ule mchanganyiko wa majani ya ukwaju uliyoyasaga hapo awali kisha changanya vizuri na asali hiyo na uanze kwa kutumia kwa kunywa asubuhi na jioni kiasi cha kijiko kikubwa cha chakula. Unaweza kutumia tiba hii kwa muda wa wiki moja mfululizo.

Zingatia
Ukihitaji kutumia tiba hii ni vyema uhakikishe kwanza umeshawahi kupima kifua kikuu na ukagundulika huna tatizo, kwani kikohozi cha muda mrefu ni moja ya dalili za kifua kikuu, hivyo kama ni kifuu kikuu ni vyema ukafuata ushauri wa daktari kwani dawa hii hutoa msaada kwa wale wenye kikohozi cha kawaida tu na si tiba ya kifua kikuu.

Kwa maelezo na ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment