Wednesday, 6 January 2016

ZIFAHAMU FAIDA ZA PARACHICHI KUANZIA JUISI YAKE MAJANI NA TUNDA LENYEWE


Hili ni tunda lenye virutubisho vingi na muhimu kwa afya zetu, na inaelezwa kuwa tunda hili huenda likawa ni mbadala wa vyakula vya nyama kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake.

Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni.

Tabibu Abdallaah Mandai anaeleza kuwa tunda hilo husaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sambamba na kujenga neva na fahamu.

Aidha, mtaalam huyo anabainisha kwamba, tunda hilo pia huweza kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu na kusheheni vitamin A, B, C na E.

Tabibu  Mandai anasema kuwa, vyakula kama nyama husababisha 'uric acid' nyingi mwilini, ambayo husababisha magonjwa mengi mwilini, hivyo tunda hili huweza kusafisha hiyo na kuitoa nje na kuondoa magonjwa pia.

“Tunda hili hufanya vizuri sana kwa magonjwa hayo na kuyamaliza, lakini pia husaidia wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi,”
alisema mtaalam huyo.

Pia majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu kunywa husaidia kuondoa matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo, kuumwa kichwa, koo (throat), tumbo, mapafu na uvimbe.

Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.

Pamoja na hayo, Tabibu Mandai anasema parachichi huweza kutumika hata katika masuala ya urembo, ambayo ni pamoja na kukuza nywele na kuokoa wale wenye tatizo la nywele zinazoanguka.

Hayo ni machache tu kuhusu parachichi, hivyo ni vizuri ukaendelea kutembelea tovuti (website) hii mara kwa mara kwa ajili ya kufahamu mambo mengi juu ya tiba asili na halisi za mimea na matunda, lakini pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba  0716 300 200 / 0769 400 800/ 0784 300 300, au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment