Tuesday, 12 January 2016

ZIFAHAMU HIZI FAIDA 5 ZA MAJANI YA MLONGE LEO

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com karibu sana tuweze kufahamishana kuhusu mimea tiba yetu tuliyobalikiwana na Mwenyezi Mungu na hapa leo ninazo sifa za matumizi ya majani ya mlonge.

1. Majani mabichi ya Mlonge huwafaa zaidi kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huku ikisaidia kuongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.

2. Majani ya mlonge yanapotengenezwa kama juisi hutumika kusafisha tumbo na kutibu magonjwa ya zinaa, lakini pia juisi inapochanganywa na asali husaidia kutibu kuharisha.

3. Pia juisi hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wale wenye presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.

4. Majani hayo hayo ya mlonge pia huweza kupakwa mwilini kwa lengo la kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.

5. Utafiti wa kisayansi umeonesha kuwa majani ya Mlonge ni chanzo kizuri cha virutubishi vingi sana ikiwa ni pamoja na vitamin C, vitamin A, Calcium na Potassium pia.

Kwa maelezo zaidi na ushauri au maoni unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasilina na Tabibu Abdallaha Mandai kwa mawasiliano yafuatayo: 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment