Monday, 1 February 2016

FAIDA ZA MAFUTA YA NAZI NA TUI LA NAZI

Nazi ni moja ya kiungo ambacho familia nyingi hasa kinamama wamekuwa wakitumia katika kuongeza ladha nzuri ndani ya vyakula.

Kimsingi nazi inauwezo mkubwa katika suala la matibabu kwani imekuwa ikisifika kuwa tiba ya matatizo mbalimbali katika miili yetu.

Leo nina hizi sababu ambazo naamini zitakufanya kupenda kutumia nazi.

Sababu ya kwanza ni hii ya nazi kuwa na uwezo mzuri wa kuwasaidia wale wenye matatizo ya uzio‘allergy’ ili nazi iweze kukusaidia katika tatizo hilo ni mhusika anapaswa kupaka mafuta ya nazi kiasi kidogo ndani ya pua yake kisha utaona upo katika hali nzuri tu hata pale utakapokuwa karibu na kile kinachokusababishia uzio ‘allergy’ kwani hautaweza hata kupiga chafya.

Pia tui la nazi lenyewe linauwezo mkubwa wa kutibu tatizo la homa ya manjano pamoja na kusaidia sana suala la kutibu afya ya damu.

Halikadhalika nazi pia husaidia sana katika kuimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni.

Hata hivyo, ili kupata matokeo mazuri katika matumizi ya mafuta ya nazi ni muhimu kuzingatia kuwa unatumia mafuta ya nazi ya asili kwa kiwango cha asilimia 100.

Pamoja na hayo, kuna manufaa mengine zaidi ya kutumia nazi, hayo ni machache tu, na kwa ufupi tu hata kile kifuu chenyewe ni tiba pia. Kama ungependa kuyajua haya zaidi endelea kuwa karibu na tovuti hii ya www.dkmandai.com kila siku. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo; 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment