Saturday, 20 February 2016

KUZIMWA KWA SIMU FEKI: BIAHARA YA SIMU YA DOROLA KARIAKOO

Wakati tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya wafanyabiashara za simu za mikononi katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam walalamikia kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki huku watuamiaji nao wakilalamikia kuwa watakosa mawasiliano kutokana na simu origino kuwa ghali.

Siku chache baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuonesha msimamo wake wa kuzifungia simu hizo baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wameelezea kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukosa wateja na hivyo kusababisha hata simu ambazo sio feki kukosa wateja na kubaini kupata hasara kubwa kutokana na azimio hilo ambapo wameziomba mamlaka husika kuongeza muda ili kuwapa nafasi ya kujipanga ili kutafuta mtaji wa kuingiza simu zinazotakiwa.

Baadhi ya watumiaji kwa nyakati tofauti  wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.

Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kuzima simu feki.

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayari imeonesha msimamo na kutangaza kuwa June 17, 2016  simu zote feki zitazimwa ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari wameshazifungia kabisa simu feki.


Chanzo: ITV

No comments:

Post a Comment