Monday, 8 February 2016

TABIBU MANDAI: NGUVU ZA KIUME SI TATIZO, TATIZO NI HOFU

Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic
UKOSEFU au upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kushindwa kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.

Miaka ya hivi karibuni tatizo hili limeonekana kuibuka kwa kasi sana miongoni mwa wanaume walio wengi, hususan vijana ambao hapo awali ilikuwa ni nadra sana kusikia kijana akilalamika kusumbuliwa na tatizo hili.

Tatizo hili limeonekana kuwakabili wanaume wengi duniani na kusababisha athari nyingi, ikiwemo suala la kuvunjika kwa uhusiano na mara nyingine ndoa.

Kimsingi tatizo hili linaweza kugawanywa katika makundi matatu, ambayo ni pamoja na umbile la mwanaume kutokuwa imara kiasi cha kupelekea mwanaume kushindwa kufanya tendo la kujamiiana au umbile la mwanaume kutokuwa na uwezo wa kusimama wakati wa tendo la ndoa.

Hali hiyo mara nyingi huwa ni matokeo ya tabia ya kujichua ‘masturbation’ kwa kipindi kirefu.

Sababu nyingine ni suala la umri, ambapo wataalam wa afya wanaeleza kuwa kadri mwanaume anavyoingia katika umri mkubwa ndipo nguvu zake za kiume hupungua.

Watu wanaozeeka wakikuambia hawana nguvu za kiume huwezi kushangaa, lakini utashangaa vijana wa leo ndiyo wanakuambia hawana nguvu za kiume.

Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na dosari za kimaumbile, ambapo kuna baadhi ya watu huweza kuzaliwa na udhaifu huo wa nguvu za kiume na wengine hupatwa na tatizo hilo mara baada ya kuzaliwa.


Ukosefu wa lishe bora nayo ni sababu ya tatizo hili, iwapo mwanaume atakuwa na historia ya kusumbuliwa na utapiamlo, huweza kuchangia madhara kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.

Sababu za kimaisha nazo huweza kuwa chanzo cha tatizo, hii humaanisha aina ya kazi ambazo mhusika anafanya, hususan za kutumia nguvu nyingi au wale ambao kazi zao ni za kusafiri sana.

Kuishi katika mazingira usiyokubaliana nayo pia huweza kuchangia tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume. Inaweza kuwa ni mazingira ya baridi au joto sana. Vyote kwa pamoja huweza kuwa na madhara katika kupunguza nguvu za kiume.

Sababu nyingine za tatizo hilo ni ajali ambazo humuacha mtu na maumivu makali, msongo wa mawazo, ulevi uliokithiri, uchovu wa mwili, matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa wataalam, magonjwa kama kisukari na kupooza mwili. ITAENDELEA tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu ya www.dkmandai.com, lakini pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment