Saturday, 19 March 2016

Hizi ndio sifa za matumizi ya tangawizi katika tiba


TANGAWIZI ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.

Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo kuweza kuiva kwa haraka zaidi.

Kutokana na tangawizi kutumiwa sana na wanawake kama kiungo hususani wanapoandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya familia au biashara wengi wanaifahamu zaidi tangawizi kama kiungo na si vinginevyo.

Wakati tangawizi ikiwa inafahamika zaidi kama kiungo, kwa upande wa tiba asili hutumika pia kama tiba na kusaidia kuondoa magonjwa mbalimbali yanayoisumbua jamii kwa sasa.

Miongoni mwa magonjwa ambayo mgonjwa anaweza kupata nafuu kutokana na kutumia tiba ya tangawizi ni pamoja na kuondoa gesi tumboni kwa wenye tatizo hilo.

Matumizi ya tangawizi pia husaidia kuwezesha mmeng’enyo wa chakula tumboni hivyo kuondoa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na matatizo ya tumbo pamoja na ukosefu wa choo.

Tangawizi inapochanganywa na mdalasini na ikatumiwa na watu walioathirika kutokana na shughuli za viwandani husaidia kulinda afya zao.

Kwa upande wa wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume na kupoteza hamu ya tendo la ndoa anapotumia tangawizi mara kwa mara wanaweza kupata nafuu ya tatizo hilo.

Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto katika mwili wa binadamu na hivyo kuamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwa akina mama wanaonyonyesha tangawizi inachochea ongezeko la maziwa na hivyo kuwaondolea changamoto ya uhaba wa maziwa unaowakabili baadhi ya akina mama wanaonyonyesha.

Matumizi ya tangawizi pia husaidia kudhibiti kwikwi na kumsaidia mtumiaji kulala usingizi mzuri zaidi ikiwa anatumia tangawizi kila mara.

Kuna baadhi ya watu husumbuliwa sana na ukosefu wa hamu ya kula. Matumizi ya tangawizi husaidia kumaliza tatizo hilo .

Tangawizi pia huwasaidia wale wenye matatizo ya kuzongwa na hali ya kichefuchefu, ili kuondosha hali ya kichefuchefu kwa kutumia tangawizi unaweza kutafuna kipande cha tangawizi na ukaona matokeo mazuri, hivyo si lazima kutumia ndimu katika kuondosha hali hiyo.

Matatizo mengine yanayoweza kutibiwa na kiungo hiki ni pamoja na matatizo ya kuhisi maumivu mara kwa mara kwenye viungo, hivyo matumizi ya chai yenye tangawizi huwa na nafasi kubwa ya kutoa ahueni kwa wenye tatizo hilo.

Kwa wenye kusumbuliwa na mafua, unapotumia chai yenye tangawizi husaidia sana katika kutibu tatizo hilo.

Wenye uzito mkubwa nao huweza kunufaika kwa kutumia kiungo hiki na wanashauriwa kutumia tangawizi kwa kuwa inasaidia kupunguza hali hiyo kwa kiwango kikubwa.

Pia tangawizi husaidia kupunguza sumu mwilini zinazotokana na ulaji wa vyakula mbalimbali, hii ni kwa sababu tangawizi huwa na uwezo mzuri wa kuondosha au kupunguza mafuta hatari yaani ‘cholesterol’ lakini pia husaidia mishipa ya damu kutoharibiwa na cholesterol. Unaweza kuiandaa kama chai na kunywa kila siku asubuhi na jioni na kufanya kuwa kinywaji chako.

Sambamba na hayo, kiungo hiki pia ni msaada kwa wanawake wenye tatizo la kupatwa na maumivu makali wakati wa hedhi. Kuna baadhi ya wanawake huhisi maumivu makali na kusababisha kukosa raha, kubana kwa misuli ya mapaja na miguu, zote hizo huweza kuwa dalili za kawaida kwa mwanamke, lakini shida ni pale maumivu hayo yanapozidi zaidi.

Tangawizi inaweza kuwa suluhisho la tatizo hilo la maumivu makali wakati wa hedhi. Unachotakiwa kufanya ni kupondaponda tangawizi mbichi, kisha chemsha maji ya kutosha kwa dakika kumi. Ongeza sukari kidogo halafu chuja. Tumia glasi moja ya maji hayo mara tatu kwa siku hususani mara baada ya kula. Matibabu hayo ni vyema yakaanza siku tatu kabla ya hedhi.

Kama utahitaji maelezo zaidi kuhusu faida za tangawizi na namna nzuri ya kutumia kiungo hiki katika matibabu basi ni vizuri ukawasiliana nami kwanza kwa namba za simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika Mandai Herbalist Clinic iliyopo, Ukonga, Mombasa maeneo ya Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment