Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 25 March 2016

Mti wa ukwaju na uwezo wake katika matibabu

UKWAJU kwa kawaida huwa na ladha fulani hivi ya uchachu, lakini pia ni moja ya kiburudishio kizuri ambacho kimesheheni virutubisho kadhaa. 

Bila shaka wengi hutumia tunda hili lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengeneza juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha.

Hata hivyo, ukwaju unaelezwa kuwa na faida nyingi kwa binadam tofauti na watu wengi wanavyofahamu.

Miongoni mwa faida za ukwaju ni pamoja na mizizi ya mti wake ambayo ikitengenezwa vizuri huwa na uwezo wa kupambana na tatizo la mkojo mchafu (U.T.I)

Mizizi hiyo husaidia kuzibua tatizo la mirija ya uzazi kuziba, lakini pia hupunguza maumivu makali kwa wanawake wakati wa hedhi au wakati wa tendo la ndoa.

Aidha, majani ya mti wa ukwaju nayo yanafaida zake katika matibabu, kwani yanapoandaliwa vizuri au kwa utaratibu unaofaa husaidia kuzuia tatizo la homa za mara kwa mara ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa malaria, kuharisha damu, homa ya matumbo sambamba na vidonda vya tumbo.

Pia majani ya ukwaju yanapokaushwa kivulini kisha kupondwa na kuwa unga laini na kisha kuunchanganya na mafuta ya nazi husaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na muwasho.

Ukwaju pia huweza kuwasaidia wenye matatizo ya miguu kuuma au kufa ganzi pamoja na kuwaka moto, ili mmea wa ukwaju utumike kama tiba hiyo itabidi uchanganywe na unga wa majani ya mkwaju na mafuta ya nazi kisha mgonjwa achue eneo husika maumivu yataisha. Fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Hali kadhalika kwa wenye tatizo la ‘athma’ (pumu) unga huo wa majani ya ukwaju ukichanganywa na na asali kisha mgonjwa kulamba husaidia kuondaoa hali hiyo sambamba na kifua kikavu.

Mbali na faida hizo za majani ya ukwaju, lakini pia magome ya mti wa mkwaju nayo ni tiba ya matatizo kadhaa.

Gome la ukwaju likianikwa kivulini kwa siku kadhaa na kisha kutwangwa na ukapatikana unga wake hiyo husaidia sana wanawake ambao hukubwa na kifafa wakati wa uzazi.

Pia gome hilo la ukwaju linauwezo wa kuwasaidia wanawake wenye shida ya kujifungua watoto wafu mara kwa mara, lakini pia huweza kuwasaidia wanawake wenye tatizo la kubeba mimba na kutoka kabla ya wakati wa kujifungua.

Namna ya kuandaa tiba hii chuna gome la mkwaju na uanike kivulini baada ya kukauka litwange vizuri, lakini kumbuka kuwa haya ni masuala yanayowahusu wanawake hivyo ni vizuri dawa hii ikaandaliwa na mwanamke tena aliyekwisha koma hedhi.

Tofauti na majani na gome la mkwaju pia juisi inayotokana na ukwaju nayo inafaida zake katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa na vitamin C, nyingi.

Matumizi ya mara kwa maera ya juisi ya ukwaju huwasaidia sana wale wenye shida ya bawasiri au mgoro, hivyo ni vyema watu wenye tatizo hilo wakatumia mara kwa ukwaju.

Juisi ya ukwaju, pia inayonafasi ya kuondoa changamoto ya miwasho sehemu za siri endapo itatumika kama kinywaji angalau kwa siku mara mbili asubuhi na jioni kwa siku kadhaa.


Juisi ya ukwaju nzito nayo huweza kutoa ahueni kwa mtu aliyeteguka Kamua ukwaju ili kupata juisi yake nzito, kisha ongeza chumvi nyingi na ukoroge vizuri kisha mchanganyiko wako huo ukishauchanganya vizuri utautumia kwa kupaka sehemu zote zenye uvimbe uliotokana na kuumia au kuteguka. Baada ya kupaka, utaacha mchanganyiko huo hapo hapo. Baada ya saa 12 paka tena, endelea hivyo hivyo hadi pale utakapoona uvimbe utakapokuwa umepungua kiasi cha kutosha au kuwa katika hali ya kawaida. Hakikisha ukwaju huo utakaobaki uliochanganywa na chumvi unaumwaga au kuvukia ili usitumiwe na watoto kwani unamadhara ikiwa mtu atakunywa ukwaju uliochanganywa na chumvi.

Lakini ni vizuri kabla hujaamua kutumia tiba hizi asili ni vizuri ukawasiliana nami kwa namba za simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:

Post a Comment