Thursday, 17 March 2016

Muembe umesheheni tiba za maradhi mengi


MAKABILA mengi hapa nchini yanapanda miembe kwa ajili ya matunda. Matunda ya miembe hufahamika kama embe ambayo ni maarufu sana hapa nchini.

Ladha tamu ya tunda hili ndiyo imefanya tunda hili kuwa na watumiaji wengi zaidi na kuliongezea umaarufu na hivyo jamii kubwa zaidi kuhamasika kulistawisha zao hilo lenye majani ya rangi ya kijani.

Tunda la embe umbo lake hutofautiana, mengi huwa na rangi ya kijani, njano au nyekundu. Embe huweza kuiva ikiwa mtini na ndio huwa nzuri zaidi, lakini kutokana na kuhofia uharibifu kutoka kwa ndege, wakulima huamua kuvuna mara tu yanapokomaa kwa kuangusha ikiwa bado hayajaiva.

Ili kugundua embe limekomaa unapaswa kuangalia mabadiliko ya rangi ambapo hubadilika kutoka rangi ya kijani na kuamia rangi ya manjano au nyekundu.

Kuna aina nyingi za embe ambazo hustawi vizuri hapa nchini miongoni mwa embe hizo ni pamoja na dodo,embe maji, bolibo na nyingine nyingi ambazo hupatiwa majina kutokana na jamii ya mazingira husika.

Tunda hili huweza kuliwa kama lilivyo, lakini pia linaweza kutengenezwa juisi ambayo mara nyingi inakuwa na virutubisho vingi .

Pamoja na hayo yote mmea huo kwa ujumla una faida nyingi za kimatibabu kuanzia mizizi , shina, magome, majani, maua na hata juisi ya tunda lake.

Juisi ya embe husaidia sana kuleta uoni mzuri kwa sababu juisi hiyo ina vitamin A ambayo huimarisha afya ya macho na kuwasaidia wale wenye macho makavu na wenye uoni hafifu wakati wa usiku 'blindness'.

Matumizi ya juisi ya embe pia huwa na faida kubwa kwa afya ya ngozi, unachopaswa kufanya ni kupaka makapi ya embe usoni na kukaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi, baada ya dakika hzio kupita utaosha uso kwa maji yanayotiririka yaani yanayotoka bombani. zoezi hilo litakusaidia sana kuonekana na ngozi nzuri pamoja na kutibu shida ya chunusi pia.

Juisi ya embe inapotumika bila kuwekwa sukari huwa ni nzuri sana kwa watu wenye shida ya kisukari kwani huenda kusaidia kurekebisha sukari ya mwili kuwa vizuri na kurekebisha mapigo ya moyo kuwa sawa na kuondoa sumu hatari mwilini

Juisi hii pia inasifika kwa kuimarisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula mwilini, pamoja na kusaidia sana kuondoa shida ya ukosefu wa choo hasa pale unapopata juisi yenye mchanganyiko wa embe na nanasi huwa nzuri zaidi kwa shida hiyo.

Ndani ya juisi ya embe kuna vitamin C, na vitamin A pamoja na 'carotenoids' ambazo zote zinapokuwa kwa pamoja husaidia sana kuimarisha kinga za mwili.

Pia ndani ya juisi ya embe hupatikana vitamin B, E. K pamoja na madini calcium, potassium, magnesium, phosphorus na iron.

Majani ya muembe hutibu maradhi ya pumu pamoja na tatizo la harufu mbaya ya kinywa, lakini pia majani haya yanapotumika vizuri huwa na uwezo mzuri wa kutibu malaria sugu. Ili kuandaa majani haya unapaswa kuchukua majani ya muembe na kuyakausha kwenye kivuli ili kutoondoa virutubisho muhimu vilivyomo ndani ya majani hayo .

Pia majani ya muembe huwasaidia watu wenye tatizo la kisukari kutokana na uwezo wa majani hayo kurekebisha kiwango cha ‘insulin’ ndani ya mwili. Unachotakiwa kufanya katika hili ni kuchemsha majani ya muembe na mhusika au mgonjwa atahitajika kunywa maji yaliyochomshwa sambamba na majani ya muembe kiasi cha glasi moja asubuhi na jioni.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa embe linauwezo wa kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo, kibofu na matiti kutokana na tunda hili kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘antioxidant.’

Matumizi ya embe pia husaidia sana kuboresha tendo la ndoa kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin E.

Kokwe la embe pia huwasaida kina mama katika matatizo ya uzazi. Twanga kokwa , unga wake tumia katika maji ya moto mara kwa mara asubuhi na jioni.

Aidha, matumizi ya magome ya mti wa mwembe nayo husifika kwa kutibu matatizo ya maumivu ya miguu kuwaka moto au kufa ganzi. Unapotumia unga wa magome ya muembe uliochanganywa na mafuta ya mzaituni na kupaka kwenye miguu husaidia kuondoa tatizo hilo.

Magome hayo pia yanapochanganywa katika uji kikombe cha chai na kuweka kiasi cha kijiko kidogo cha chai na kutumiwa na mwanamke mwenye tatizo la kupatwa na maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa au maumivu wakati wa hedhi husaidia kuondoa matatizo hayo.

Mizizi ya mwembe nayo, inatibu maradhi kadhaa na hivyo huufanya mti wa mwembe kuzidi kuwa na faida nyingi kataika matibabu.

Kama utahitaji maelezo zaidi ya faida za mti wa mwembe na namna ya kuutumia katika matibabu basi usisite kuwasiliana nami kwa namba simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika Mandai Herbalist Clinic tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment