Saturday, 5 March 2016

ZIFAHAMU HIZI SIFA ZA MSTAFELI KATIKA TIBA

STAFELI ni tunda ambalo hustawi zaidi katika ukanda wa kitropiki, hapa nchini hupatikana zaidi katika mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya, Morogoro na baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam.

Stafeli pia linafahamika kama topetope, lakini kwa lugha ya kiingereza hufahamika kama ‘sour sop’ na mara nyingi mti wa mstafeli huwa si mrefu sana.

Licha ya tunda lake kuwa na ladha nzuri , lakini pia mti wa mstafeli unasifika kwa kuwa na uwezo katika matibabu na ni miongoni mwa miti ambayo inaelezwa kutumiwa na wazee wetu katika kutibu magonjwa mbalimbali kipindi cha miaka kadhaa iliyopita.

Miongoni mwa magonjwa ambayo mti huo huweza kuyatibu hata sasa ikiwa utatumiwa vizuri ni pamoja na matatizo ya wanawake hususani sehemu za siri.

Wanawake wenye matatizo ya kutokwa na maji yenye muwasho au yenye asili kama maziwa mtindi sehemu zao za siri wanaweza kutibiwa na mti huo na kupona kabisa.

Mara nyingi wanawake hukumbwa na matatizo hayo mara kwa mara kutokana na maumbile yao . Magonjwa hayo yamekuwa ni changamoto kwa wanawake kutokana na kuchangia athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine huweza kusababisha hata matatizo ya uzazi pia ikiwa hayatapata tiba sahihi kwa uharaka zaidi.

Aidha, mti huo huweza kurejesha sehemu za siri za mwanamke zilizoharibika hususani wakati wa uzazi, ambapo mwanamke husika atahitajika kuchemsha majani ya mti wa mstafeli na kuyaacha yapoe kisha atatumia maji hayo kuoshea sehemu husika.

Si hayo pekee ambayo huweza kutibiwa na mti huu wa mstafeli bali hata matatizo ya vidonda vya tumbo nayo huweza kutibiwa kwa kutumia majani ya mti wa mstafeli.

Magome ya mti wa mstafeli nayo hutumika kama tiba pia na hasa hutibu matatizo ya uvimbe au vidonda. Ili magome hayo yakusaidie katika matatizo hayo unapaswa kutafuta gome la mti wa mstafeli na kuliponda kisha bandika gome uliloponda sehemu yenye tatizo (uvimbe au kidonda) kidonda kitapona.

Pamoja na faida hizo, lakini pia majani ya mti wa mstafeli yanaposagwa na kutumika kama chai kwa kuchanganywa na maji ya moto na kutumiwa kila siku asubuhi na jioni husaidia kuimarisha kinga za mwili na kumuepusha mhusika kukumbwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Mbali na kutibu matatizo hayo, pia mstafeli umekuwa ukisadikika kwa kuwa na uwezo wa kutibu matatizo ya saratani.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Saratani Nchini Uingereza (NIR) iliyofanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mnamo mwaka 1976 na kubaini kuwa mizizi, majani na tunda la stafeli vyote huweza kutoa ahueni kwa wagonjwa wa saratani.

Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki kilichopo nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la bidhaa asilia nao ulibaini kuwa stafeli linauwezo wa kumsaidia mgonjwa mwenye saratani ya tumbo.

Ukiachilia mbali tafiti hizo, kuna utafiti mwingine ambao ulifanywa na Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani ambao walibaini kuwa licha ya mstafeli kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa watu wenye matatizo ya saratani, lakini pia tunda hilo ni tiba ya mfadhaiko wa mwili.

Kimsingi mstafeli ni miongoni kati ya miti ambayo bila shaka yoyote unaweza kuuweka katika orodha ya miti dawa yako ambayo umekuwa ukiitumia au kuifahamu. Hivyo kama ulikuwa haufahamu vizuri ni namna gani sahihi ya kuutumia mti huu ili uweze kuwa tiba kwako basi unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu zilizopo hapo juu ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu faida za mti wa mstafeli au mtopetope.

Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment