Saturday, 16 April 2016

Daraja la Kigamboni kufunguliwa rasmi leo

Muonekano wa daraja wakati wa matengenezo (Picha na Mtandao)
Wakati Watanzania wakisubiri kwa hamu kukamilika kwa Daraja la Kigamboni lililojengwa kwa kushirikia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambalo linatarajiwa kufunguliwa Jumanne ijayo 

Tayari kuna hizi dondoo muhimu zimeletwa kwa Watanzania watakaotumia daraja hilo
Muonekano wa kuingilia daraja la Kigamboni pamoja na vyumba vya kukatia tiketi (Picha kwa hisani ya Mtandao)
Mambo yasiyotakiwa Daraja la Kigamboni
1) Kwenda mwendo kasi

2) Kupitisha magari yenye uzito unaozidi tani 10 kwa siku za mwanzo yaani leo Jumamosi

3) Kupitisha mikokoteni na maguta

4 Utupaji wa taka ovyo 

5) Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

6)Madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela hawaruhusiwi kuegesha eneo hilo ili kuepusha msongamano na foleni eneo la daraja.

No comments:

Post a Comment