Saturday, 30 April 2016

Zifahamu hizi faida za asali na mdalasini leo


MDALASINI ni miongoni mwa viungo vinavyotumika kuongeza radha katika vyakula, pia kikitumika ipasavyo ni tiba maridhawa ya maradhi mbalimbali.

Asali nayo ni moja ya vyakula vilivyo katika hali ya kimiminika ambacho hutumiwa na watu wengi kwa kulamba au kuipaka katika vyakula ukiwemo mkate.

Pia wapo wanaoitumia kuweka katika chai badala ya sukari, hususan kwa wagonjwa wa maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ambao wameshauriwa kutumia kiasi kidogo cha sukari na chumvi.

Leo katika makala haya tunaangalia namna ya kuchanganya asali na mdalasini ili kupata tiba ya maradhi mbalimbali. Mdalasini ni tiba ukitumia magome, mafuta na majani yake.

Unapotumia unga wa gome la mmea huu unaweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba. Mwanaume unapaswa kutumia vijiko viwili vya gome la mdalasini kwa kuuchanganya na asali. Utumie mchanganyiko huo baada ya mlo wa jioni.

Matumizi ya mchanganyiko huu husaidia pia wanawake kuhamasisha kizazi. Aidha, husaidia pia kuondoa sumu mwilini ‘cholesterol’.

Si hayo tu mdalasini pia husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi .Tatizo la kujaa gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu au kutapika pamoja na kuharisha linatibiwa kwa kutumia mdalasini.

Hali kadhalika maumivu ya viungo nayo huweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia mchanganyiko huo kwa sababu mmea huo una utajiri mkubwa wa madini ya ‘magnesium’ ambayo pia huimarisha afya ya mifupa.

Ndani ya mdalasini kuna virutubisho vyenye uwezo wa kulinda afya ya kinywa na kupambana na mashambulizi dhidi ya bakteria. Hivyo, inatajwa kuwa ni mojawapo ya kinga ya asili ya fizi na meno.

Si hayo tu matumizi ya mdalasini pia husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na hivyo kufanya kuwa kiungo chenye faida kwa wale wenye shida ya kisukari hususan kisukari aina ya pili 'type 2 diabetes'.

Kwa wale watoto wenye tatizo la kujisaidia choo ndogo kitandani, huweza kusaidiwa kwa kutumia kiungo hiki pia.

Ili kumtibu kwa tiba hiyo mzazi unapaswa kumpatia mtoto wako kipande (gome) moja la mdalasini atafune kila asubuhi mchana na jioni kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu mfululizo.

Pia mdalasini huwasaidia wanawake ambao hupatwa na matatizo ya maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.  Ikiwa mwanamke anasumbuliwa na tatizo hilo atahitaji kutumia mdalasini kama suluhisho la hali hiyo.

Unachopaswa kufanya ni kupata unga wa mdalasini kijiko kimoja na kisha weka kwenye maji ya moto glasi moja kisha changanya vizuri. Ukimaliza ongeza na asali kiasi kisha tumia mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.

Mafuta ya mdalasini nayo husaidia kuondoa tatizo la fangasi hususan aina ya 'Candida' Mchanganyiko wa asali na mdalasini husaidia pia kuimarisha kinga za mwili, mtu menye tatizo hilo akitumia mdalasini humsaidia kutopatwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Mbali na hayo, mdalasini pia husaidia kupunguza unene kwa kuwa una uwezo mkubwa wa kurahisisha mzunguko wa damu mwilini.

Mtu mwenye tatizo la mafindofindo ‘tonsillitis’ huweza kupata ahueni ikiwa atatumia mdalasini ipasavyo.

Unachopaswa kufanya ni kupata unga wa mdalasini kijiko kimoja, weka kwenye glasi ya maji kisha changanya na asali vijiko viwili baada ya hapo kunywa mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki moja.

Asali na mdalasini inapotumiwa kwa pamoja husadia  kuboresha usagaji wa chakula tumboni na hivyo kurahisisha upatikanaji wa choo laini na huzuia tumbo kujaa gesi, lakini pia mchanganyiko huo husaidia kuongeza nguvu mwilini na huchangamsha akili.

Hayo ni machache kuhusu mdalasini na asali, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kunipigia simu kwa namba  zifuatazo: 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com pia unaweza kutembelea ofisini kwetu tupo Ukonga, Mongo la Ndege jijini  Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment