Wednesday, 20 April 2016

Maajabu ya tikitimaji katika tiba


TIKITIMAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana katika maeneo mbalimbali nchini tofauti na miaka iliyopita.

Hali hiyo inaashiria kuwa tunda hilo linawatumiaji wengi, huenda ni kutokana na faida zake auladha yake nzuri.

Tunda hili kisayansi linajulikana kama ‘Citrullus lanatus’  na ukuaji wake huwa ni wa kutambaa.

Lina umbo linalofanana na tufe au yai. Asili ya  tunda hili ni Afrika Magharibi na Kusini.

Inakadiriwa kuwa asilimia 92 ya tunda hili ni maji, lakini licha ya kuwa na maji hayo yenye ladha nzuri pia hili faida kadhaa katika masuala ya afya hususan pale linapotumika ipasavyo.

Tikitimaji ni chanzo cha virutubisho mbalimbali ndani ya mwili wa mwanadamu ikiwa ni pamoja na vitamin A ambayo husadia kuimarisha afya ya macho.

Pia lina vitamin C, ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na hivyo kumfanya mhusika kutoshambuliwa na magonjwa mara kwa mara pamoja na kusaidia kulinda afya ya meno na fizi.

Tikitimaji lina ‘amino acid ’ ambayo husaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa, na hivyo kumwondelea mtumiaji hatari ya kukumbwa na shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2013 kwenye jarida moja nchini Marekani, ulionesha kuwa ulaji wa tikitikimaji kwa wenye uzito mkubwa unapunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu.

Faida nyingine ya tikitimaji husaidia kuondoa maumivu ya misuli, hivyo kuwa msaada kwa wanamichezo hususan waliojijengea utaratibu wa kutumia tunda lenyewe au juisi yake.

Pamoja na hayo, tikitimaji husaidia kulinda afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamin A na C, linapewa sifa hiyo kutokana na kuwa na vitamin A ya kutosha ambayo husaidia katika ukuzaji wa tishu za mwili ikiwemo nywele na ngozi.

Kimsingi karibu kila kitu kwenye tunda hili kina faida kiafya ukianzia mbegu zake majani hadi tunda lenyewe.

Juisi yake pia husaidia kutoa nafuu kwa wale wenye matatizo ya mawe katika figo au kibofu.

Tikitimaji pia husaidia kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mwili hii ni kutokana na kuwa na madini ya 'potassium' pamoja na vitamin C na A.

Sababu hiyo inatosha kusema kuwa tunda hili huweza kuwa msaada kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume au wenye tatizo la kuwahi kufika kileleni kwa sababu mzunguko wa damu unapokuwa vizuri mwilini basi huchangia hata viungo vya uzazi vya mwanaume kuwa na mhemko kwa haraka zaidi.

Pamoja na hayo, mbegu za tikitimaji zinapokaangwa na kusagwa kisha mhusika kutumia kwa kuchanganya kwenye maji ya moto na kisha kunywa husaidia kuondoa maumivu wakati wa kutoa haja ndogo (mkojo)

Sanjari na hayo, matumizi ya tunda hili pia husaidia kuwakinga wanaume dhidi ya saratani ya kibofu kutokana na tunda hilo kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘lycopene.’ Hoja  hii inapewa nguvu zaidi na ripoti ya mwaka 2009 kuhusu uhusiano kati ya chakula na hatari ya saratani ya kibofu.

Mbegu za tunda hili tamu zinakiwango kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia kubadili chakula kuwa katika mfumo wa nishati.

Mbegu hizo pia zina uwezo wa kuboresha mmeng’enyo wa chakula pamoja na mfumo wa fahamu, huku zikisaidia kuimarisha afya ya ngozi kwa mtumiaji.

Kwa maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa tikitimaji unaweza kuwasiliana  nami kwa namba za simu O716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika kwenye kliniki yetu ya Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege Dar es Salaam.Makala kama hizi pia unaweza kuzipata kupitia Gazeti la TAMBUA linalotoka kila siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment