Saturday, 7 May 2016

Epuka mambo haya wakati wakumlisha mtoto chakula

HABARI za weekend mpendwa msomaji wa www.dkmandai.com, karibu sana katika muendelezo wetu wa kuhakikisha unapata elimu ya afya kila siku ikiwemo tiba asilia.

Leo nimeona tuwakumbuke watoto ili kuwahakikishia usalama wao katika mazingira ya kula.

Ukweli ni kwamba familia nyingi kwa sasa zimekuwa zikiishi na kinadada wa kazi (House Girl) ambao ndio kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishiriki katika kuwatunza watoto nyumbani na kuhakikisha wanakula vizuri na kushinda katika hali ya usalama.

Hivyo ninayofuraha kukwambia wewe mzazi pamoja na dada wa nyumbani au mlezi mambo haya machache ya kuzingatia katika kuhakikisha usalama wa mtoto wakati wa kula;

Jambo la kwanza hakikisha haumuachi mtoto mdogo na chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa, kama utasahau na kumuacha mtoto katika hali hiyo huweza kusababisha mtoto akapaliwa.

Jambo la pili, ambalo nalo ni muhimu kulizingatia ni pamoja na kuepuka kumpa mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka endapo utafanya hivyo kutakuwa na nafasi kubwa ya mtoto kumpaliwa.

Pia epuka kumpa mtoto chakula ambacho kinaweza kumkaba au kumpalia hususani karanga, maindi, zabibu n.k.

Jambo lingine la msingi na kuzingatiwa ni kuhakikisha unapoma joto la chakula kabla ya kumpa mtoto usipofanya hivyo unaweza  kumuunguza mtoto mdomo.


Mbali na hayo yote, pia usafi katika maandalizi ya chakula cha mtoto ni muhimu zaidi, hii ni kuanzia mhusika anayemlishaji na hata mtoto mwenyewe anayelishwa hili ni muhimu sana sana kwa afya ya mtoto.

Mandai Herbal Clinic inapenda kukujuza kwamba kama unateseka na magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu sasa ni mwisho, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unafika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na upate matibabu sahihi kwa kutumia tiba asilia za mimea na matunda. Wasiliana nasi sasa kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment