Saturday, 28 May 2016

Fahamu siri ya kitunguu swaumu kiafya


KITUNGUU swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali.

Mbali na kiungo hicho kutumika kunogesha vyakula pia kikitumiwa ipasavyo ni tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Miongoni mwa matatizo ya kiafya yanayoweza kumpata nafuu mgonjwa kutokana na kiungo hicho ni pamoja na ugonjwa wa kifua.

Ugonjwa wa kifua huchangiwa na mifereji inayoingiza hewa katika mapafu inapopata maambukizi na kusababisha mgonjwa kukohoa kikohozi chenye sauti mara kwa mara, huku kikiambatana na makohozi mazito.

Kitunguu swaumu pia husaidia kutoa ahueni kwa wenye matatizo ya ngozi hususan yenye vilenge lenge ambapo dalili zake ni madoa meupe yenye magamba (huchunika kama ngozi iliyoungua) mikononi, miguuni, shingoni au usoni. Hivyo matatizo yote hayo huweza kufanyiwa suluhisho kwa kutumia kitunguu swaumu.

Matumizi ya kitunguu swaumu ni msaada pia kwa watu wenye matatizo ya kukosa choo kwa muda wa siku mbili au zaidi anaweza kutibiwa kwa kutumia kiungo hiki.

Aidha, kiungo hiki pia kinasaidia kupunguza shida ya kubanwa na pumu au kushindwa kupumua, lakini pia kitunguu swaumu husaidia kutibu majeraha yatokanayo na kuumwa na wadudu kama ng'e ambapo ili utumie kiungo hiki kama tiba utapaswa kukisaga kisha utabandika sehemu yenye tatizo.

Maumivu ya kiuno nayo huweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia kiungo hiki, lakini pia kitunguu swaumu kinaweza kutumika kama tiba ya kusafishia vidonda kutokata na uwezo wake wa kuua vijidudu au bakteria.

Ili kutumia kiungo hiki katika hili mhusika atapaswa kusaga kitunguu swaumu na kukibandika sehemu ya kidonda kwa muda usiopungua dakika kumi na baadaye kutoa. Ni kizuri hata kwa vidonda ndugu.

Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vinaelezwa kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa wenye maambukizi ya bakteria, fangasi pamoja na virusi tofauti tofauti.

Kiungo hiki pia kina sifa za kutoa unafuu kwa wenye tatizo la saratani za aina mbalimbali ikiwemo ya tumbo na utumbo mkubwa hii ni kutokana na tafiti kuonesha idadi ndogo ya watu wenye matatizo ya saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia kiungo hiki mara kwa mara.

Hata hivyo, si vizuri kutumia kiungo hiki bila kupata ushauri wa wataalamu wa tiba zitokanazo na mimea au tiba asili wanaotambulika kisheria.

Mbali na hayo, kitunguu swaumu huweza kutumika kama njia ya kuboresha afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji kuwa mrembo. Kwenye haya masuala ya urembo kiungo hiki huweza kuwa msaada kwa wale wenye matatizo ya chunusi.

Ili kumaliza shida hiyo ya chunusi mhusika atachanganya kitunguu swaumu kilichosagwa pamoja na kijiko cha juisi ya ndimu. Kisha chukua pamba na upake sehemu iliyoathirika.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment