Saturday, 7 May 2016

Fahamu uwezo wa tango katika tiba


BILA shaka mara nyingi umekuwa ukisikia wataalam wa afya na lishe wakisisitiza matumizi ya mboga za majani na matunda kwa kuwa vina imarisha afya na kumkinga mtumiaji dhidi ya maradhi mbalimbali.

Tango ni miongoni mwa matunda yenye manufaa kwa afya ya mwanadamu kwa kuwa limesheheni virutubisho vingi muhimu katika kujenga na kuulinda mwili.

Miongoni mwa virutubisho hivyo ni pamoja vitamin B1, B2, B3, B4, na B6, lakini pia ndani ya tango kuna madini ya chuma, 'potassium' na 'zinc.' ambayo ya umuhimu mkubwa katika mwili wa mwanadamu.

Mtumiajia anaweza kula tango baada ya kuliosha au kunywa juisi yake iliyoandaliwa katika hali ya usafi.

Unapokula tunda hili ni vizuri ukala hadi maganda yake iwapo unaweza, kwa sababu yana vitamin na madini mengi. Hata ukila bila maganda bado inafaa pia.

Matumizi stahiki ya tunda hilo husaidia kumkinga mtumiaji na maradhi ya saratani, kutibu vidonda vya tumbo na maradhi ya ngozi.

Unapoweka maji kwenye beseni na kutumia tango kuoshea uso husaidia kuondoa chunusi , majipu na michaniko mwilini. Kwa ujumla tunda hili husaidia kuleta uzuri wa ngozi.

Ngozi inahitaji tango ili kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia (taratibu bila kutumia nguvu)  vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika inasaidia maajabu baada ya siku chache.

Lakini pia tango huweza kusaidia tatizo la midomo kukauka. Katika hili inatakiwa kuchukuwa kipande cha tango na kusugulia mdomoni taratibu bila kutumia nguvu, itasaidia baada ya siku kadhaa kuondokana na tatizo hilo.

Kwa wale wenye shida ya mikono yenye kuchubuka na iliyokauka wanashauriwa kutumia tango kupaka mikono (kuoshea)  au kupaka mwili wote.

Aidha, tango husaidia kwa wale wenye tatizo la uoni hafifu nyakati za usiku 'night blindness' ambapo mhusika atahitajika kutumia vipande vya tango vilivyokatwa kwa mtindo wa duara na kuweka juu ya macho angalau kwa dakika tano usiku kabla ya kulala.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO), linasema kila sekunde tano mtu mmoja duniani anakuwa kipofu. Aidha, shirika hilo linasema kila dakika moja mtoto mmoja duniani anapata upofu.

Pamoja na hayo, WHO inakadiria kwamba zaidi ya watu milioni saba hupata matatizo ya macho na kuwa vipofu kila mwaka, huku ikielezwa kuwa asilima 80 ya kesi za upofu huweza kuepukika. Hivyo, matumizi ya tango huweza kutoa ahueni kwa matatizo ya macho pia.

Tango ni moja ya njia nzuri zinazosaidia kuondoa makovu. Unachotakiwa ni kuponda tango na kisha kutumia mchanganyiko wake kwa kupaka kwenye  kovu. Hii husaidia kulainisha makovu na ikiwa utatumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

Matango pia husaidia kusafisha au kuzuia ugonjwa wa ini pamoja na figo na koo, huku likisaidia kuondoa uchovu wa mwili na kumuongezea nguvu mhusika.

Tunda hili hali kadhalika husaidia kwa wale wenye tatizo la baridi yabisi (rheumatism), kuvimba miguu kwani huondoa 'uric acid'.

Pamoja na hayo, kwa wale wanaosumbuliwa na kisukari, na kupungua uzito wa mwili wanashauriwa kulifanya tunda hili sehemu ya mlo wao.

Pia tango linaweza kutoa msaada katika shughuli za usafi. Chukua kipande cha tango sugulia viatu vyako, inaelezwa kuwa husaidia kuving'arisha lakini mbali na hilo pia inaaminika hinaweza kusaidia kusafishia vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu matumizi ya tango unaweza kuwasiliana nami kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, au Barua Pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment