Saturday, 28 May 2016

Fahamu kuhusu huu mmea wenye uwezo wa kukutibu magonjwa mbalimbali

Mti wa Mwingajini
MWINGAJINI ni moja ya mmea (mti) mdogo ambao faida zake kiafya huenda ni kubwa kuliko muonekano wa mti huo.

Inawezekana jina la mti huu likawa ni geni masikioni mwako, lakini huenda ukiuona kwa sura unaweza kuutambua vizuri na pengine utakuwa unapatikana hata katika mazingira yako ya kila siku.

Kisayansi mti huu unafahamika kama ‘Senna Occidentalis’ lakini jina ambalo linaumaarufu mkuwa wa mtii huu ni hili la ‘Cofee Senna ‘ .

Moja ya matatizo yanayoweza kupata ahueni kwa kutumia mmea huu ni pamoja na matatizo ya kuota kinyama sehemu ya haja kubwa yaani ‘mgolo’ pamoja na kumaliza maumivu ya viungo sambamba na kutoa ahueni kwa wenye kisukari.

Mbegu za Mwingajini
Nchini Jamaica hutumia mbegu za mmea huu wa mwingajini kwa kumaliza matatizo tajwa hapo juu. Ambapo mhusika atapaswa kuchukua mbegu hizo na kuzisaga kisha kutumia kwenye maji moto jambo ambalo hutoa mafanikio kwenye matatizo hayo.

Pamoja na hayo, majani ya mwingajini husaidia pia kutibu majeraha yanayotokana na kuumwa na wadudu kama vile ng’e.

Hata hivyo, si vizuri kutumia mmea huu kama tiba pasipo kupata ushauri wa kina kutoka kwa mtaalam wa tiba asili. 

Kwa maelezo zaidi au mengine zaidi kuhusu mmea huu unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment