Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 31 May 2016

Soma hapa vyakula na matunda vitakavyokuondolea tatizo la kusahauTatizo la kusaha ni moja ya tatizo ambalo huwakumba watu wa rika mbalimbali hususani wale wenye umri mkubwa.

Kuna baadhi ya watu wenye tatizo hili la kusahau sana hadi kufikia hatua ya kusahau hata kula na ukimuuliza leo umekula au hujala mtu wa namna hiyo anaweza kukujibu kwamba 'sikumbuki vizuri'

Pia kuna baadhi ya watu wenye umri mdogo lakini wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili na hata kupelekea wakati mwingine kushindwa kufanya vizuri katika masomo kutokana na kusahau kile kinachofundishwa darasani/ shuleni/ chuoni.

Mandai Herbal Clinic inakujuza haya yafuatayo yatakayo kusaidia kutunza kumbukumbu.

Kwanza kabisa ni matumizi ya maua ya komamanga, ambapo utahiitaji kukusanya machipukizi ya maua ya komamanga na kuyakausha katika kivulina baadaye kuyasaga hadi yawe unga na kutunza unga huo katika chupa safi yenye mfuniko.

Kisha utakuwa ukitumia nusu kijiko cha chai cha unga huo katika maji ya uvuguvugu mara tatu kwa muda wa mwezi mmoja.

Njia nyigine ni kutumia, rozimeri hii husaidia kutunza kumbukumbu ambapo mhusika atatakiwa kutengeneza kikombe kimoja cha chai ya majani ya rozimeri (mabichi au makavu) kisha ongeza asali kijiko kimoja cha mezani. Koroga, kunywa , fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu.

Pilipili Manga, chukua kijiko cha chai cha unga wa pilipili manga kisha changanya na kijiko kimoja cha chai cha asali nautmie kwa kulamba polepole kila asubuhi na jioni.

Hali kadhalika unapokula wali na maziwa mtindi kila mara huweza pia kuimarisha uwezo wako wa kutunza kumbukumbu zaidi.

Sambamba na hayo pia ni vyema kuzingatia kupata muda wa kupumzika vizuri pamoja na kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi yote hayo yatakusaidia pia kuongeza uwezo wako wa kutunza kumbukumbu vizuri.

Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata ufumbuzi wa magonjwa yako yanayokusumbua. Wasiliana sasa na  Tabibu Abdallah Mandai kwa simu zifuatazo,0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment