Friday, 13 May 2016

Tabibu Mandai afafanua faida za kitunguu maji kiafya

Tabibu  Abdallah  Mandai akizungumza na waandishi wa habari (Picha na Maktaba)
KITUNGUU maji ni moja ya kiungo ambacho hutumika karibu kila siku katika mapishi, lakini kiungo hiki pia kina nafasi yake katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Leo Tabibu Mandai ameona akupatie dondoo muhimu kuhusu kiungo hicho nimeona na namna ya kukitumia katika matatizo mbalimbali ya kiafya.

Tabibu Mandai anasema kitunguu kikitumika vizuri husaidia sana kuondosha dalili zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na ile hali ya kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye moyo, lakini pia kitunguu husaidia kumuepusha mhusika dhidi shinikizo la damu 'blood pressure' au mshituko wa moyo 'heart attack'

Kitunguu maji pia huweza kutumika katika kuongeza damu mwilini kutokana na kuwa na utajiri wa madini chuma ndani yake, hivyo kiungo hiki huweza kuwa ni msaada mzuri kwa watu wenye anemia.

Kitunguu pia husaidia kuongeza uwezo wa kongosho kuzalisha ‘insulin’ ya kutosha na hivyo kupelekea mwili kuwa katika kiwango cha sukari kinachohitajika mwilini.

Aidha, kitunguu pia kina sifa ya kutibu matatizo ya ngozi, kinachofanyika katika swala hili ni kutengeneza juisi ya kitunguu kisha paka sehemu iliyoathirika na utaona mafanikio.
Kitunguu maji
Kwa wale kina dada wenye shida ya kukatika kwa nywele basi unapotumia juisi ya kitunguu maji husaidia sana kuondosha tatizo hilo na kuzifanya nywele kukua vizuri na kuonekana kuwa na afya nzuri. Kinachopaswa kufanyika katika hili ni kutumia juisi hiyo ya kitunguu maji na kupaka kwenye shina ya nywele kwa kila wiki mara mbili. Fanya hivyo kwa miezi kadhaa.

Pia kitunguu maji kinauwezo wa kupambana na vijidudu vinavyosababisha kifua kikuu TB pamoja na maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani U.T.I.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini  Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment