Monday, 9 May 2016

Tumia maua ya boga kama unatatizo la mtoto wa jicho


MAUA ya boga hutokana na mboga za maboga na maua hayo hutokea pindi mmea huo unapoelekea kuzaa maboga.

Sehemu kubwa ya Watanzania wamekuwa wakitumia maua hayo kama mboga ambapo huchanganya na majani ya mboga hiyo na kuongeza mvuto ladha zaidi kwenye mboga hiyo.

Pamoja na maua hayo ya maboga kutumika kama mboga, pia maua hayo huweza kutumika kama sehemu ya dawa hususani kwa wale wenye tatizo la mtoto wa jicho.

Tatizo la mtoto wa jicho hutokea pale ambapo mtu anapokuwa amejeruhiwa katika chembe hai zinazohusika na utengenezaji wa lensi ya jicho. 

Jeraha hilo huweza kuchangiwa na matumizi ya muda mrefu ya jicho husika na hivyo kusababisha hali hiyo, hata hivyo mara nyingi tatizo hili huwakumba watu wenye umri mkubwa zaidi.

Mbali na sababu hiyo, tatizo hili pia huweza kuchangiwa na majeraha ya moja kwa moja kwenye jicho. Mfano ajali.

Wengine huweza kupata maradhi haya kutokana na sababu za kurithi hii huchangiwa na hitilafu katika utengenezwaji wa chembe hai zinazohusika na kuiunda lensi ya jicho.

Kimsingi maradhi haya hutokea pale ambapo chembe hai zinazotengeneza lensi ya jicho kujeruhiwa na hivyo kuunda lensi yenye mapungufu na ambayo haina uwezo wa kupokea mwanga wa taswira kama vile ulivyoingia kwenye jicho kwa kupitia sehemu ya mbele.

Madhara makubwa yanayotokea kwenye maradhi haya ni usambazaji mbovu wa mwanga huu wa taswira unapofika kwenye lensi. Hii husababishwa na kutokuwa na unyoofu wa mazingira katika ukuta wa lensi uliotokana na kujeruhiwa kwa chembe hai zake zinazoundwa.

Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kuwa kadri binadamu anavyoendelea kuongezeka kiumri lensi ya jicho/macho hupunguza uwezo wake wa kufanya kazi, hii ni kutokana na kushindwa kwa lensi kutanuka na kusinyaa vizuri ili kufanikiwa kuelekeza mwanga ule wa taswira kuelekea kwenye retina.

Mtu mwenye tatizo hili huweza kupata shida hii kwenye jicho moja tu, lakini kwa waliowengi hupata kwenye macho yote mawili yote.

Maua ya maboga ndiyo hutumika katika tiba hii, ambapo mhusika atachukuwa maua ya maboga na kutengeneza juisi yake kisha atatakiwa kupaka juisi hiyo kwenye kope za macho asubuhi na jionii kwa muda wa mwezi mmoja. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmai. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment