Tuesday, 3 May 2016

Tumia mbegu za papai kama una tatizo hili

PAPA ni miongoni mwa matunda yanayopatikana hapa nchini, lakini pia ni moja ya matunda ambayo yana watumiaji wengi.

Miongoni mwa watumiaji wa tunda hili wamekuwa wakitumia kama tiba ya kulainisha choo au ya kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Sasa leo ni vyema ukatambua kuwa mbali na faida hizo za papai, pia mbegu zake huweza kutumika kama tiba ikiwa zitaandaliwa vizuri.

Mbegu za papai zinaposagwa na kukaushwa katika kivuli na kisha kuwa katika hali ya unga laini ni tiba ya minyoo. Ugonjwa huo ambao hupatikana sana katika maeneo yenye hali ya usafi duni.

Maambukizi ya ugonjwa huu hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya askaris.

Minyoo huchukua sehemu kubwa ya virutubisho mwilini kutoka kwenya sehemu ya chakula ambacho bado hakijameng'enya vizuri katika utumbo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuuliza kupitia simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment