Thursday, 5 May 2016

Umuhimu wa maziwa mtindi kwa afya

TATIZO la tumbo kujaa gesi ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua wengi na kusababisha maumivu ya tumbo au tumbo kuwa na miungurumo ya hapa na pale.

Tatizo hili huchangiwa sana na aina ya vyakula unavyokula hususani vile vyenye mafuta mengi, lakini pia husababishwa na vinjwaji unavyokunywa hasa soda au bia.

Kwa kawaida aina ya vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakul,  hivyo huleta matatizo kwenye mfumo mzima wa usagaji chakula.

Maziwa ya mtindi huweza kuwa suluhisho la tatizo hili na ni vizuri ukatumika ule mtindi halisi, maziwa hayo husaidia sana kurekebisha mfumo wa usagaji wa chakula na kuufanya kuwa mwepesi.

Pia papai husaida sana tatizo hili kwa sababu tunda hilo huenda kurekebisha mfumo wa usagaji wa chakula na uwezo huo hutokana na uwepo wa kirutubisho cha ‘enzyme’ ambacho hupatikana ndani ya papai.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza  kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment