Monday, 23 May 2016

Unajua maajabu ya iliki katika tiba? Soma hapa


HAPA duniani Mwenyezi Mungu ametujalia vitu mbalimbali ambavyo vikitumiwa vizuri vinaweza kuwa na thamani katika maisha ya kila siku hususan katika kujenga afya zetu.

Iliki ni moja ya viungo vinavyofahamika na wengi. Watu hukitumia kila siku katika shughuli za mapishi kama ya chai. Pia kiungo hicho kina faida zake katika afya.

Asili ya iliki ni nchini India. Lakini kwa sasa kiungo hicho kinastawishwa na kupatikana katika maeneo mbalimbali duniani.

Iliki inavirutubisho vingi, huku miongoni mwavyo ni pamoja na vitamin A, C pamoja na madini ya 'calcium', 'potassium', 'sodium', 'copper', 'zinc' 'magnesium' na madini ya chuma.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kilimo na Lishe nchini Marekani,  iliki ina carbohydrates 68g, protin 11g pamoja na nyuzinyuzi kiasi cha 28g.

Moja ya faida za matumizi ya iliki ni kusaidia kuipa figo uwezo mzuri figo wa kuondoa taka mwili, huku ikisaidia kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Iliki pia husaidia kuondoa hali ya kiungulia pamoja na tatizo la gesi tumboni. Aidha, kiungo hicho kinatoa msaada kwa watu wenye tatizo la kukosa choo au kupata choo kwa shida  constipation  kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa na Chuo cha Pharmacy of King Saud kilichopo Saud Arabia, kiungo hicho kilionesha uwezo wa kuboresha mishipa ya damu kwenye moyo na hivyo kuulinda dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Vilevile iliki inasaidia kuondoa tatizo la maradhi ya kinywa hususan kuweka sawa harufu ya kinywa, lakini pia matumizi ya kiungo hicho husaidia kutibu vidonda vya mdomoni na matatizo ya kinywa kwa ujumla.

Pia iliki ina uwezo wa kutibu matatizo ya  maambukizi kwenye njia ya mkojo sanjari na kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya kujamiana.

Iliki pia ina uwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua na kikohozi, huku ikisifika kwa kuondoa maumivu ya viungo vya mwili.

Mbali na hayo, iliki pia ina uwezo wa kukabiliana na dalili za matatizo ya saratani na shinikizo la damu. Hali kadhalika iliki pia ina uwezo wa kuondoa dalili za tatizo la pumu na matatizo kwenye mfumo wa hewa.

Kiungo hicho pia husaidia kufifisha hali ya kichefuchefu na hivyo kumsaidia mhusika kutotapika endapo atakuwa ana sumbuliwa na hali hiyo.

Mwenye kusumbuliwa na maumivu ya koo anaweza kutumia iliki, lakini ni vema ikachanganywa na unga wa mdalasini kisha ichemshwe vizuri na baadaye mhusika wa tatizo hilo atapaswa kunywa asubuhi na jioni angalau ndani ya wiki mbili tatizo litakuwa limekwisha.

Kwa leo naomba tuishie hapa, kama utahitaji kuyajua mengi zaidi kuhusu matumizi ya iliki unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800. Au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege.

No comments:

Post a Comment