Wednesday, 4 May 2016

Viazi mviringo vitakusaidia dhidi ya vidonda vya tumbo na michirizi kwenye ngozi


WENGI wetu tumekuwa tukitumia viazi mviringo kama chakula ambacho huweza kupikwa au kutengenezwa kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘chips’

Lakini leo ni vyema ukafahamu matumizi mengine ya viazi hivyo mbali na kutumika kama chakula tu.

Viazi hivyo vinapopondwa na kubandikwa juu ya tatizo lolote la ngozi au bawasira huweza kutoa ahueni ya tatizo au kumaliza tatizo kamisa endapo mhusika ataitumia tiba hiyo kikamilifu na mara kwa mara.

Aidha, matumizi ya juisi ya kiazi kilichopondwa husaidia kutatua matatizo kama baridi yabisi pamoja na vidonda vya tumbo.

Pamoja na hayo, kiazi pia ni ‘tonic’ ya ngozi, kinachotakiwa kufanyika katika hili ni kunawia juisi yake na machicha yake utayabandika kila mahali juu ya ngozi na itasaidia kuondoa makunyanzi yote ya uzee pamoja na kulainisha ngozi.

Kama hayo hayatoshi basi ni vyema ifahamike pia kuwa maganda ya viazi hivyo pia yanauwezo wa kuondosha madoa ya chunusi au michirizi sehemu mbalimbali za mwili.

Kama utakuwa na swali au unahitaji kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya viazi mviringo kama tiba basi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment