Monday, 2 May 2016

Zabibu ni matunda yanayoweza kukuokoa dhidi ya maradhi

ZABIBU hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukua katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.

Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana zaidi mkoani Dodoma.

Matunda haya huwa na rangi ya nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi tumezoea kuyaona matunda haya yakiwa na rangi  nyeusi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula  na Kilimo Duniani (FAO) linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu zote duniani hutumika kutengenezea  mvinyo na asilimia 27 pekee huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2 ikifanywa kukaushwa kwa ajili ya matumizi mengine.

Pamoja na hayo, wengi hawafahamu umuhimu wa tunda hili na faida zake katika mwili wa binadamu, hivyo leo kupitia makala haya utaweza kuzifahamu baadhi ya faida za zabibu.

Zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo, lakini pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana  na sababu hii hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi (stroke).

Matumizi ya zabibu husaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu mwilini, hivyo kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepuka ugonjwa wa anemia pia.

Mbali na hayo, tafiti mbalimbali zanaonesha kuwa zabibu zinauwezo wakuukinga mwili dhisi ya saratani kutokana na kuwa nakirutubisho kiitwacho ‘antioxidants’ ndani yake ambayo huweza kupambana na aina mbalimbali za saratani ndani ya mwili. Miongoni mwa aina hizo za saratani ni pamoja na saratani ya kibofu, tumbo, koo na saratani ya matiti.

Ulaji wa zabibu pia husaidia kumaliza tatizo la ukosefu wa haja kubwa, kwani ndani ya sabibu kuna asili ya nyuzinyuzi ambazo ni muhimu katika umeng’enyaji chakula na kumsaidia mhusika kupata choo kwa urahisi zaidi.

Matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.

Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Divai pia husaidia bacteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo (normal flora) kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo kuwa rahisi.

Mbali na hayo ulaji wa punje za zabibu zisizopungua angalau tatu kwa siku husaidia kulinda afya ya mfumo mzima wa damu na nyama za moyo.

Kimsingi faida za zabibu ni nyingi, kwani husaidia pia kuongeza uoni mzuri hususani kwa wazee endapo watatumia tunda hili mara kwa mara.

Hayo ni machache kati ya mengi kuhusu zabibu, lakini kama unahitaji kufahamu faida nyingine za matunda haya basi unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 Au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisini kwetu tupo Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege jijini Dar  es Salaam.

No comments:

Post a Comment