Thursday, 26 May 2016

Zijue hizi faida 5 za kutumia asali mara kwa mara


HABARI za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com naamini msomaji wangu utakuwa upo vizuri napenda kukukaribisha kwa pamoja tuweze kuzifahamu hizi faida 5 za asali katika matibabu.

Asali hufanya kazi mbalimbali mwilini ikiwa ni pamoja na kuponya maradhi, lakini pia husifika kwa kuwa na uwezo wa kuimarisha kinga za mwili.

Faida 5 za kutumia asali

1. Kwanza asali huweza kulainisha jipu na kuondosha usaha

2. Pili huweza kutuliza maumivu ya tumbo na kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni. Ili tumbo lako liweze kufanya kazi yake vizuri ni vyema ukajizoesha kula asali kijiko kimoja kila siku asubuhi kabla ya kula chochote

3. Husaidia kutibu vidonda hususani vile vya wazi na majeraha yatokanayo na moto

4. Pia asali husaidia kwa wale wenye matatizo ya kifua na mapafu.

5. Asali inauwezo mzuri pia wa kuimarisha kinga za mwili

Unaweza pia kupata masomo haya ya mimea tiba na vyakula kutoka kwa Tabibu Abdallah Mandai kupitia gazeti la TAMBUA linalotoka kila siku ya Ijumaa.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment