Wednesday, 11 May 2016

Zipate hizi faida za kahawa leoKAHAWA ni moja ya kinywaji ambacho kimekuwa kikipendwa sana na watu mbalimbali nchini.

Karibu maeneo mengi utakutana na vijiwe hivi vya kahawa, huku watu wakiendelea kunywa na kubadilishana mawazo ya hapa na pale inaweza kuwa kuhusu siasa, michezo na hata masuala ya uhusiano pia.

Mara nyingi wanywaji wakubwa wa kinywaji hiki ni wanaume kuliko wanawake.

Miongoni mwa faida za kinywaji hiki ni pamoja na kumchangamsha mhusika na kumfanya kujihisi vizuri.

Kwa mujibu wa Jarida la Afya ya Mifumo ya Mishipa ya Fahamu la Uingereza lilichapisha ripoti kuhusu kinywaji hicho na kueleza kuwa, inapunguza hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa fahamu kwa wazee.

Kutokana na hili inaonesha kuwa wazee wanapokunyw kinywaji hiki wanaweza kuimarisha zaidi mifumo ya fahamu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment