Wednesday, 29 June 2016

Anza kutumia majani ya mstafeli kama unamatatizo haya ya kiafya..

Stafeli ni tunda ambalo hupatikana katika mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya, Morogoro na baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam.

Tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani.

Kwa mujibu wa Jarida la Kemia na madawa la nchini Marekani la mwaka 2010 linaeleza kuwa tunda hili la Stafeli au Mtopetope kuwa lina uwezo wa kuangamiza chembe hai zenye saratani pasipo kusaleta madhara katika mwili.

Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza (NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976 na kubaini kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vyote vina uwezo wa kutibu saratani.

Mbali na faida ya tunda lenyewe pia majani yake yamekuwa yakielezwa kuwa na faida mbalimbali mwilini ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu pamoja na kutoa ahueni kwa matatizo ya uvimbe na majipu.

Ili majani haya yaweze kukusaidia katika matatizo hayo unapaswa kutumia kuyaandaa kama chai kutokana na majani freshi ya mstafeli na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi mmoja. Inashauriwa hiyo chai unywe nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni.

Kwa maelezo zaidi jinsi ya kutumia majani ya mstafeli kwa manufaa zaidi unaweza kuwasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba +255716 300 200/ +255769 400 800/ +2550784 300 300, Barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment