Friday, 17 June 2016

Fahamu faida 12 za tikiti
Tikiti ni tunda ambalo  lina faida  nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa chanzo kizuri cha ‘Protini’ , nyuzinyuzi, pamoja na madini ya ‘Calcium’, ‘Phosphorus, ‘potassium’ magnesium ‘Chuma’,Vitamin A, B6, C.

Kutokana na virutubisho hivyo tunda  hili linaingia kwenye orodha ya matunda ambayo huweza kuimarisha afya ya misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kumuondoa mhusika katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Faida 12 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Husaidia kushusha na kutoa nafuu kwa wenye shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake

Karibu Mandai Herbal Clinic, tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo: 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment