Wednesday, 22 June 2016

Fahamu matatizo ya uvimbe mfuko wa uzazi


Tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa uzazi 'fibroid' huweza kusababisha mwanamke kushindwa kupata mtoto kwasababu uvimbe huu unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari au sehemu mayai yanapotengenezwa.

Uvimbe huu pia unaweza kuzuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi  pia hufanya mfuko wa kizazi ukaze na hivyo kushindwa kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

Tunapaswa kujua kuwa wanawake wengi wana 'fibroid' ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili ni ngumu kufahamu.

Kwa mantiki hiyo wataalam wa afya hushauri kufanya uchunguzi wa afya  mara kwa mara ili kuweza kushughulikia haraka matatizo kama haya.

Moja ya matatizo ambayo huleta huzuni na uchungu ndani ya familia ni pamoja na hili swala la familia kushindwa kubahatika kupata watoto.

Hali hiyo hupelekea huzuni ndani ya nyumba, chuki, lawama, kejeli na kushutumiana na kusababisha hata talaka pia kati ya wanandoa

Lakini leo nimeona nianze kuzungumzia hili tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi jambo ambalo mwishowe hupelekea ugumu wa mama kushika ujauzito.

Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni yanayoambatana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment