Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 27 June 2016

Fahamu mmea wa mnanaa kwa afya yako

Mnanaa ni mmea ambao unapatikana  katika nchi mbalimbali ikiwemo za hapa Afrika Mashariki, huku wengi wakiutumia mmea huu kwa kuupanda kama maua katika nyumba zao pamoja na bustanini.

Mmea huu huwasidia kinamama ikiwemo kuondoa maumivu wakati wa hedhi, kizazi kuuma pamoja na kuongeza maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha.

Aidha, mnanaa pia husaidia watu wenye tatizo la misuri inayokaza ama kustuka , kutuliza maumivu ya sikio, kutuliza maumivu, sambamba na husaidia homa ya manjano.

Mnanaa pia husaidia maradhi ya koo, minyoo kwa watoto,kuzui kichefuchefu na kutapika, kutoa gesi tumboni na kuzuia kuharisha na matatizo ya tumbo.

Hata hivyo, mnanaa huleta auheni kwenye  maradhi ambayo ni pamoja na matatizo ya meno, ambapo mhusika hupaswa kusukutua au kutafuna mmea huo, huku ukifahamika kwa kuwa dawa nzuri ya kulinda meno yasiweze kumeguka  au kung’oka  na kuvuja damu kwenye fizi.

Kama utapenda kufahamu mengi zaidi usisite kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/+255 0769 400 800/+255 784 300 300.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment