Thursday, 2 June 2016

Fahamu umuhimu wa haya makundi ya chakula

Kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo huwa tunakula katika maisha yetu ya kila siku bila kujali faida zake wala madhara yake hii ni kwa sababu wengi wetu tunakula kile tunachokipata na si tunachopenda kula yaani unaweza kusema tunakula kutokana na majaaliwa ya mwenyezi Mungu.

Kimsingi vyakula tunavyokula huwa na umuhimu mkubwa na kazi mbalimbali ndani ya miili yetu ikiwa ni pamoja na kuupatia mwili virutubisho mbalimbali muhimu.

Mwili wa binadamu unahitaji vyakula vya aina mbalimbali ili kuupatia mwili aina tofauti tofauti ya virutubisho. 

Vyakula vimegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na kazi zake mwilini. Kwa kawaida mtu anatakiwa kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali ili kuuwezesha mwili kupata virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika.

Mtu anayepata mlo wenye virutubisho vyote muhimu huyu tunaweza kusema kuwa anapata ‘mlo kamili’ ambao ni muhimu sana mwilini hususani kwa watoto kwani husaidia ukuaji wao. Vile vile mlo kamili ni muhimu pia kwa wazee na wagonjwa kwani husaidia kujenga mwili.

Mgawanyiko wa Vyakula.
Vyakula vya wanga.
Hivi ni vyakula muhimu sana katika mwili kwani huupatia mwili nguvu. Vyakula vyenye wanga ni pamoja na mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele n.k.

Wanga pia hupatika kupitia viazi vitamu, magimbi, ndizi na hata asali .

Vyakula vyenye protini
Hivi ni vyakula muhimu sana katika kujenga mwili pamoja na kusaidia kujenga kinga za mwili. Vyakula vyenye protini ni pamoja na samaki, mayai, maziwa, maharage, soya, kunde, njegere, choroko, mbaazi na hata njugu mawe.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kila wakati kwani tutaendela kukuletea muendelezo wa makundi mengine ya vyakula pamoja na faida zake mwilini. Tafadhari endelea kuperuzi tovuti yetu hii mara kwa mara kadri uwezavyo ili kupata taarifa zaidi kila siku.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment