Wednesday, 29 June 2016

Fahamu umuhimu wa kula uyoga kimwili

Uyoga ni moja ya mboga ambayo imekuwa ikiliwa na baadhi ya watu hapa nchini, lakini je, umewahi kuwaza kuwa mboga hiyo inaweza kuwa dawa .

Majibu ya maswali hayo yanapatikana kutoka katika hii stori kutoka nchini Taiwan, ambapo wao uyoga kwao hutumika kama dawa ya kupunguza unene.

Kwa miaka sasa uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya kupunguza unene katika wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini ‘Taiwan’.

Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la mawasiliano ya mazingira umebainisha kuwa madini ya yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kuwa na uzito mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.

Imeelezwa kuwa madini hayo ya  yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani

Wataalam wanasema kuwa sayansi hiyo ni nzuri, lakini matumizi yake hayapaswi kuwa ya holela kwani uchaguzi wake huhitaji wajuzi wa uyoga unaofaa kuliwa pekee.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba +255716 300 200/ +255769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment