Tuesday, 21 June 2016

Zifahamu faida za tangawizi


Tangawizi tumekuwa tukiwa nayo karibu kila siku katika maisha yetu ya kawaida na mara nyingi wengi wetu huitumia kama kiungo kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye chai

Kiungo ambacho hutuliza matatizo mbalimbal ndani ya mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuupatia mwili joto.

Licha ya kuwa tiba ya magonjwa kama kikohozi na mafua, tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa kama uchovu.

Huongeza hamu ya kula chakula. kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.

Unywaji wa tangawizi husaidia uzalishaji wa mate mdomoni  kuongezeka kwa mate mdomoni husaidia kutengeneza vichocheo muhimu vinavyosaidia wakati wa kula, na hupunguza pia uwezekano wa magonjwa ya meno.

Husaidia kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu pia hupunguza kichefuchefu na kutapika na  huwasadia sana wale watu waliotumia sana madawa na kuwa na  sumu nyingi mwilini.

Pia humsaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu      

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment