Monday, 20 June 2016

Fahamu uwezo wa embe kiafya

Ukiamua kuzungumzia matunda yenye faida kimwili naamini huwezi kuacha kulitaja embe
Tunda hilo ambalo huzaliwa na mti ambao mara nyingi huonekana  yenye ukubwa wa wastani na rangi ya kijani kibichi kila wakati.

Kabla ya kuzaliwa embe mti huu huwa na maua ya rangi ya waridi hadi nyeupe katika vishada vya maua na msimu wake ni kati ya mwezi Desemba hadi Aprili.

Tunda la embe umbo lake hutofautiana, mengi yao huwa aidha na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu.

Embe inaweza kuiva ikiwa mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ambao hula tunda hili, wakulima huamua kuvuna mara tu inapokomaa kwa kuangusha ikiwa bado haijaiva.


Utagundua kuwa embe imekomaa kwa kuiangalia rangi kwani hubadilika kutoka rangi ya kijani hadi ya manjano au nyekundu.

Kuna aina nyingi za embe kama vile embe dodo, embe mali, embe bolibo,  embe nuka,  embe kidney, embe Julie manzano na  kadhalika.

Watu wengi hupenda kula embe ikiwa imeiva lakini ulaji wake ikiwa bado mbichi huweza kutumika kupunguza hali ya kichefuchefu.


Nyama ya tunda hili ni tamu pia ina virutubisho kwani ni  chanzo cha upatikanaji wa vitamini A na C mwilini.

Maembe pia yanaweza kugandishwa, kukaushwa kwa jua na kuweza kutumika siku nyingi zijazo.

Embe  husaidia kuimalisha ngozi,kupambana na magonjwa ya moyo na ‘stroke’huimalisha kushiliki tendo la ndoa

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:

Post a Comment