Thursday, 30 June 2016

Hiki ndicho kitakachotokea mwilini mwako ikiwa utatumia dafu ndani ya wiki

MAJI ya dafu ni muhimu moja ya kinywaji ambacho huburudisha, lakini pia kinywaji hiki kinapotumika mara kwa mara huweza kuwa na manufaa mbalimbali kiafya.

Leo napenda tufahamishane baadhi ya faida ambazo huweza kupatikana kwa kutumia maji ya dafu.

Miongoni mwa faida za maji ya dafu ni pamoja na kuongeza virutubisho vya aina tano ambavyo vyote huwa na umuhimu ndani ya mwili wa binadamu. Virutubisho hivyo ni pamoja na madini ya ‘calcium’, ‘magnesium’, ‘potassium’, ‘phosphorous’ na ‘sodium’.

Dafu pia husaidia kupunguza tatizo la msukumo mkubwa wa damu mwilini, katika hili maji ya dafu hushauriwa kutumika asubuhi kabla ya kutumia chakula chochote au kinywaji.

Pia dafu linaelezwa kuwa na faida ya kupunguza hali ya uchovu hususani hangover , sambamba na hayo matumizi ya maji haya ya dafu pia husaidia kupunguza matatizo ya maumivu wakati wa kupata haja ndogo (mkojo).

Matumizi ya dafu pia husaidia kupunguza uzito kwa wale wenye uzito mkubwa wa mwili, lakini pia huongeza hamu ya kula kutokana na uasilia wake.

Mbali na faida hizo, maji ya dafu pia husaida kuimarisha kinga za mwili pamoja na kusaidia kuua bacteria mbalimbali wakiwemo wale ambao huchangia tatizo la U.T.I.

Kuna mengine mengi kuhusu faida za dafu na maji yake lakini kwa sasa niishie hapa naomba endelea kutembelea mtandao huu mara kwa mara na utayapata hayo mengine kila siku, lakini pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba +255716 300 200/ +255769 400 800/ +255784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment