Thursday, 16 June 2016

Sababu 10 zitakazokufanya uanze kutumia maji ya limao leo

Kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa za kiafya mwilini, lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu huenda kukawa na faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. 

Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili, mbali na  vitamini C ndimu ina vitamini ‘B-complex’  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na nyuzinyuz (fiber) 

Inaelezwa kuwa ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko hata tofaa 'apple' au  zabibu.


Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . 

Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na ladha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida isipokuwa wale wenye matatizo ya upungufu wa damu (anemia) ambao huweza madhara  zaidi.


Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao


1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi’acid’ lakini likiwa tumboni huwa alkali ‘alkaline’ na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.


Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula 
kusukumwa vizuri.


2: Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.


3: Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant ‘antioxidant’ ambayo inasaidia kuondoa ‘Free Radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani ‘cancer’.


 4: Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya 'citrus fruits’ inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemicischemic stroke’ hasa kwa wanawake.


5: Usafishaji wa Mwili na Damu

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo  ini na mfumo wa chakula.


 6: Kurekebisha Sukari katika Mwili

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.


7: Dawa ya Kikohozi na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.


8: Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.

Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.


 9: Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale ambao wanataka kupungua uzito.


 10: Kuondoa Harufu ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.Kwa maelezo zaidi na ushauri mpigie Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment