Monday, 13 June 2016

Sababu 6 zinazochangia mwanaume kushindwa kutungisha mimba


Kuna wanaume wengi wamekuwa wakishindwa kuwapatia wanawake ujauzito bila wao kujua ni nini sababu ya hali hiyo.

Katika jamii nyingi hususani hizi zetu za kiafrika inapotokea hali ya wanandoa kukosa mtoto au watoto basi lawama na mashaka huelekezwa zaidi kwa wanawake, licha ya kwamba tatizo huweza kuwepo hata kwa kinababa.

Leo Jumamosi ninazo hizi sababu ambazo huweza kumfanya mwanaume kuwa katika uwezekano mkubwa wa kushindwa kusababisha ujauzito kwa mwanamke.

1. Unywaji wapombe na matumizi ya madawa
Kama wewe ni mwanaume na unamipango ya kusababisha ujauzito kwa mke wako ni vyema ukajitahidi sana kukaa mbali na matumizi ya pombe pamoja na madawa, hii ni kwa sababu matumizi ya vitu hivyo huasababisha upotevu wa uwezo wa mbegu kusababisha ujauzito kwa mwanamke, lakini matumizi ya vitu hivyo huleta madhara mengine makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuweza kuchangia ugumba kwa kinababa na kupoteza uwezo wa kushiriki vizuri tendo la ndoa.

2. Magonjwa Mwanaume inapotokea akawa amezongwa na magonjwa mbalimbali hali hiyo huweza kuchangia sana mwanaume kuwa na uwezo mdogo wa kusababisha ujauzito kwa mawanamke na miongoni mwa magonjwa hayo ni kama kisukari, matatizo ya figo, shinikizo la damu, saratani pamoja na msongo wa mawazo pia.

Kwa hayo yote huweza kupelekea mwanaume kushindwa kumpatia mwanamke mimba au kutokuwa na uwezo mzuri wa kushiriki tendo au kuwa na mbegu hafifu na ambazo hazina ubora, licha ya kwamba hali si lazima kumtokea kila mwanaume.

3. Uzito
Uzito wako pia unaweza kuwa chanzo cha tatizo hili la uzazi kwa kina babana kusababisha kupoteza uweza wa kusababisha mama kushika ujauzito, kwa mantiki hiyo ni vyema baba ukawa na uzito wa wastani kabla ya kufika wakati wa kuhitaji kupata mtoto katika ndoa yako na ili kuwa na uzito wa kawaidia unapaswa kuzingatia mpangilio wa mlo wako pamoja na kuzingatia kufanya mazoezi pia, lakini hii hali ya uzito mkubwa si sababu pekee inaweza kumfanya mwanaume kushindwa kumpatia mwanamke mimba bali hata kuwa na uzito mdogo zaidi kuna wakati huweza kuwa sababu ya tatizo.

4. Joto
Hali ya ujoto sana katika sehemu za uzazi wa mwanaume huwa haitakiwi sana kwani hufubaza uwezo wa mbegu za kiume pale joto linapozidi sana hivyo ni vyema kuvaa nguo ambazo hazina joto sana na ziwe zile zenye asili ya pamba kuliko mpira.

Pia kwa wale wanaume ambao kazi zao huwafanya kukaa kwa muda mrefu huweza kukumbwa na tatizo hili ikiwa hawatakuwa makini mfano wa kazi hizo ni zile za ofisini na madereva hawa ni vyema wakajenga utaratibu wa kusimama kila baada ya mda na kuzunguka kidogo ili kuepusha joto la mwili kuzidi sehemu za siri.

Halikadhalika kwa wale wanaofanya kazi za uokaji wa mikate nao huweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili hivyo ni vyema kuwa na tahadhari kubwa.

5. Uvutaji wa sigara.
Hii nayo ni moja ya sababu ambayo huweza kuleta hali nguma ya baba kusababisha ujauzito kwa uathiri mbegu za uzazi za kiume pia, inaelezwa kamba jinsi unavyovuta sigara mara kwa mara basi ndivyo unavyozidi kuwa katika hatari zaidi ya tatizo hili, hivyo ni vizuri ukajitahidi kujiepusha na matumizi ya sigara kutokana nakuwa na madhara hayo.

6. Magonjwa ya ngono
Hii ni moja ya sababu ambayo huchangia sana mwanaume au hata mwanamke kushindwa kupata mtoto, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na kisonono. kaswende, haya huweza kuwa sababu ya tatizo pia hivyo ni vyema kuyaepuka kwa kuhakikisha unajikinga kwa kutumia kondom kila unaposhiriki.

Hata hivyo, ni vyema watu walio katika mahusianao wakajenga utaratibu wa kupima magonjw hayo mara kwa mara ili kuepuka kuambukizana ndani ya nyumba.

Kwa maelezo zaidi na ushauri mpigie Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment