Monday, 20 June 2016

Tambua faida ya mlo kamili kiafya

Siku zote afya ya mwanadamu hutegemea sana kinga aliyonayo mwilini,kinga ambayo hujengwa na ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vya aina mbalimbali kwa namna ambavyo Mungu ametujalia.

Kwa kawaida mwili unapaswa kujilindi wenyewe dhidi ya maradhi ya kila aina  ukiwa na kinga imara, lakini pale inapobidi basi dawa ndipo huchukua nafasi yake katika kuusaidia mwili kupambana na magonjwa.

Kutokana na hayo yote inamaanisha kwamba mwili unahitaji mlo kamili ambao unajumuisha matunda, mboga za majani, nafaka na vyakula vingine vya asili, kwa sababu kila unachokula kina faida yake mwilini lakini siyo tu kula chochote kinachoitwa chakula bali ule chakula ambacho kitakuwa na maslai katika afya ya mwili wako.

Idadi kubwa ya watu wamekuwa hawapati chakula sahihi, badala yake wanakula vyakula ambavyo si tu ni hatari kwa afya zao, bali pia hudhoofisha kinga ya asili ya mwili na hivyo kuufanya mwili kubaki dhaifu na unaoweza kupatwa na magonjwa wakati wowote  chanzo kikuu cha kushuka kwa kinga ya mwili kinasababishwa na ulaji wa vyakula visivyo sahihi ambavyo ndivyo vinavyopatikana kwa wingi kila mahali, hasa sehemu za mijini vyakula visivyofaa ndivyo vinavyotangazwa na kunadiwa kwenye vyombo vya habari kuwa bora.  Hivyo kuna kila sababu ya kubadili mpangilio wako wa vyakula sasa ili ulinde afya yako.

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa ushauri zaidi juu ya mpangilio wa mlo wako piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment