Tuesday, 28 June 2016

Tumia vyakula hivi pale unaposumbuliwa na tatizo la tumbo kujaa gesi


Tatizo la tumbo kujaa gesi ni moja ya matatizo ambayio yamekuwa yakiwakabili watu wengi mbaya zaidi wengi wao hushindwa kutambua nini chanzo cha tatizo hilo.

Tumbo linapojaa gesi mara nyingi huambatana na miungurumo ya tumbo ya hapa na pale, pia tumbo huweza kuchafuka na wakati mwingine mhusika hujikuta akihisi maumivu.

Kwa kiasi kubwa tatizo hilo huchangiwa na vyakula ambavyo mhusika atakuwa amekula. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo.

Miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha tatizo hili ni pamoja na  soda, bia pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi.

Mara nyingi vyakula hivyo vinapofika tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakula na hivyo huwa kikwazo katika mfumo mzima wa usagaji chakula.

Ili kuepuka tatizo hili unashauriwa kutumia vyakula vifuatavyo:

PAPAI
Baadhi ya tafiti zilizowahi kufanyika zinaainisha kuwa ndani ya papai kuna  ‘enzyme’ ambayo husaidia kurahisha usagaji wa chakula tumboni na hivyo kulifanya tunda kuwa katika hali nzuri ya kutokujaa gesi.

MAZIWA MTINDI
Maiwa mtindi nayo huweza kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Maziwa hayo ni mazuri ikiwa hayajachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza ladha. Inaelezwa kuwa bakteria asilia wanaopatikana kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mzuri.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba +255716 300 200/ +255769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment