Wednesday, 22 June 2016

Umuhimu wa mazoezi kwa mama mjamzito

Mama mjamzito anapofanya mazoezi, humsaidia kutanua misuli ya kiuno na ile ya njia ya uzazi. Hivyo mazoezi  huipa nguvu na uvumilivu  misuli wakati wa kujifungua.

Aidha, misuli inapokuwa mwepesi, huwa ni rahisi mwili huo kurudi katika umbile lake la awali mapema mara baada ya kujifungua.
 
Mjamzito anapofanya mazoezi, huufanya moyo wake kupata mapigo mazuri na kuchochea mzunguko mzuri wa damu, huku mazoezi pia yakimsaidia mama mjamzito asiongezeke uzito na kumuepusha na shinikizo la damu.

Kuna mazoezi ambayo ni mazuri kwa mama anayetarajia kupata mtoto, licha ya kuwa baadhi ya mazoezi huenda yasiwe na matokeo mazuri kwa mama ambaye amebakiza siku chache za kujifungua.

Hivyo, mama hutakiwa kuhakikisha anawasiliana na daktari wake kabla hajafanya uamuzi wa aina ya mazoezi ya kufanya.

Miongoni mwa mazoezi ambayo huweza kumsadia mama ni pamoja na kutembea, ambako humsaidia mjamzito asitetemeke magoti na kifundo cha mguu.

Halikadhalika mazoezi ni muhimu ya mwili ni muhimu sana katika kipindi chote cha ujauzito kwani yanaweza kumsaidia mama mjamzito kuondokana na uwezekano wa  kukumbwa na tatizo mbalimbali  kwa sababu mazoezi hayo husaidia kupunguza kiwango cha sukari kwa kutumia glukosi kwa ajili ya nguvu ya kufanya mazoezi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment