Friday, 24 June 2016

Yafahamu haya maajabu ya mlonge katika tiba leo


Hapa nchini kuna miti ya aina mbalimbali ikiwemo ile inayotambulika na jamii kutokana na umaarufu na ipo mingine ambayo pia haifahamiki kabisa.

Mfano wa baadhi ya miti ambayo inafahamika kiasi kwamba hata ukiitaja katika kundi la watu basi ni lazima asilimia kubwa watakuwa wanaifahamu ni pamoja na mti wa muarobaini na mbuyu, ambayo imekuwa ikifahamika kama miti dawa na imekuwa ni msaada mkubwa kwa wale ambao hufahamu matumizi yake.

Miti mingine ambayo pia ni dawa ni ile ya aina ya Miyombo ambayo pale inapokauka huweza kutumika kama kuni hii ni kutokana na miti hiyo kuaminika kuwa kuni zake hutoa mkaa mzito na wenye kudumu kwa muda mrefu.

Pamoja na faida na umaarufu wa miti hiyo, lakini hapa Tabibu Abdallah Mandai anabainisha mti mwingine ambao umekuwa na historia ndefu katika masuala ya tiba.

Tabibu Mandai anasema mti huo ni mti wa mlonge ambao pia ameufanyia utafiti kwa muda mrefu na ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi ya binadamu.

"Tafiti zangu ama vyanzo vikubwa vya utabibu wa leo vinakubaliana kwamba huu ndiyo ule mti ambao Mussa alioneshwa na Bwana katika Kitabu cha Kutoka sura ya 15 na uliotumika katika kuyatibu maji ya pale Mara" anasema

Anafafanua kuwa, licha ya mti huo kutibu magonjwa mbalimbali, mlonge pia ni dawa ya inayowekwa kwenye maji na kuua wadudu na kusafisha maji ya kunywa.

"Funga fundo dogo la unga wa majani ya mlonge katika kitambaa safi, tumbukiza kwenye ndoo ya maji, utakuwa umeua wadudu na kuyasafisha maji yote" anasema Tabibu Mandai.

Hata hivyo, mbali na hayo Tabibu Mandai inabainisha kuwa pia mbegu za mti wa mlonge zinauwezo wa kutuliza magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na  shinikizo la damu.

Anasema kwamba mbegu za mlonge hali kadhalika zina uwezo wa kuwasaidia wenye tatizo la baridi yabisi na uvimbe wa magoti , kifua kikuu (TB), kisukari Ukimwi, kukosa usingizi, magonjwa ya zinaa, harufu mbaya mdomoni, vidonda vya tumbo, majipu pamoja na homa ya matumbo.

Magonjwa mengine yanayoweza kupata ahueni kwa mbegu hizo ni malaria sugu, pumu, matezi, saratani na maumivu ya mwili huku mafuta ya mbegu hizo yakiwa ni dawa ya kuchua maumivu ya mwili.

Pamoja na hayo, Mandai anaeleza kwamba gome la mlonge linapochemshwa na kuwa laini husaida kwa wenye  ugonjwa wa bandama na kuwapa nafuu, ini, maumivu, tetenasi na kupooza, huku akiongeza kuwa majani ya mlonge yanapopikwa huliwa na kusaidia katika kupambana na uhaba wa vitamin C kwani upungufu wa vitamini hiyo husababisha damu kuvuja kwenye fisi za meno.

Hali kadhalika, majani ya mlonge yanapowekwa kwenye kidonda au uvimbe husaidia, lakini juisi inayotokana na majani ya mlonge ikichanganywa na asali huwa ni dawa nzuri kwa magonjwa ya macho.

Baada ya kuyafahamu hayo yote ni vizuri pia tukafahamu kuhusu mizizi ya mlonge, ambapo Mandai anasema mizizi ya mti mchanga wa mlonge ni tiba nzuri ya mishipa ya fahamu, kifafa, nyongo, baridi yabisi sugu na kujaa maji.

Mandai ni mtaalam wa tiba asilia mwenye uzoefu katka utoaji wa huduma za tiba asili, anapatikana Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege jijini Dar es Salaam wasilina naye kwa simu namba + +255716 300 200/+255769 400 800/ +255784 300 300 a u barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment