Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 14 June 2016

Yafahamu matatizo ya kiafya yanayoweza kutibiwa na limao

LIMAO ni moja ya tunda ambalo linafahamika sana, ni tunda ambalo mara nyingi hutumika zaidi jikoni kwa ajili ya kukata shombo fulani fulani ya baadhi ya mboga mfano samaki.

Kwa kawaida limao huwa na ladha ya uchachu, lakini pamoja na kuwa na ladha hiyo tunda hili limekuwa na faida pia za kiafya.

Limao ni kinga ya magonjwa ya kinywa na meno, kwani juisi hiyo huwasaidia wale wenye shida ya kutokwa na damu kwenye fizi, lakini pia huondoa tatizo la harufu mbaya kinywani na husaidia kung'arisha meno.

Aidha, juisi ya limao pia ni kinga nzuri ya matatizo ya usagaji wa chakula pamoja na ukosefu wa choo 'constipation' inaaminika kuwa kiasi cha matone kadhaa ya limao katika kinywaji chako huwa ni msaada mkubwa wa matatizo hayo ya umenge'nyaji wa chakula na ukosefu wa choo, lakini pia unapokunywa juisi ya limao mara baada ya chakula chako cha mchana au usiku husaidia kurahisisha mzunguko mzuri wa damu ndani ya mwili.

Hayo ni machache kuhusu limao kwa mengine mengi unaweza kuendelea kufuatilia tovuti hii mara kwa mara au unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kusoma makala za tiba kama hizi kupitia gazeti la TAMBUA linalotoka kila siku ya Ijumaa

No comments:

Post a Comment